ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 22, 2018

GAVANA WA MJI WA IMO NIGERIA KUWASOMESHA WANAFUNZI YATIMA WA TANZANIA BURE NCHINI NIGERIA

Gavana wa mji wa imo nchini Nigeria, Rochas Okorocha, akimpongeza mwanafunzi wa darasa la Sita, Anati Mujib wa Shule ya Msingi Makumbusho, anayefanya vizuri katika masomo yake darasani, wakati Gavana huyo alipoitembelea shule hiyo akiambatana na mwenyeji wake Mkurugenzi wa 

Taasisi ya Tulia Trust Fund, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson, (kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na kuchagua baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu ili kuwasomesha katika shule na Chuo chake kilichopo nchini Nigeri. Gavana huyo akiwa shuleni hapo alitoa zawadi ya Dola 100 kwa kila mwanafunzi aliyeongoza kimasomo katika darasa la tano, Sita na Saba kwa kila mmoja, na Dola 200 kwa mwanafunzi wa Kidato cha tatu Shule ya Sekondari Makumbusho, Raymond Kalistus, anayefanya vizuri kimasomo darasani, ambapo pia alitangaza kumdhamini mwanafunzi huyo wa Darasa lasaba, Abdul Ausi kwa kumsomesha Sekondari hadi Chuo Kikuu kuanzia sasa kutokana na kufiwa na wazazi wotewawili. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Gavana akimkabidhi zawadi ya Dola 100 mwanafunzi, Anati Mujibu.
Gavana akikumbatiana kwa furaha na mwanafunzi, Abdul Ausi wa daeasa la saba aliyetangaza kumsomesha kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, kwa kuchagua nchi yeyote aipendayo kwenda kupata elimu.
Gavana akisalimiana na baadhi ya wanafunzi Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaosoma katika shule hiyo
Gavana akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiaga kuondoka shuleni hapo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitafsiri hotuba ya mgeni wake Gavana wa mji wa Imo nchini Nigeria, wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya msingi Makumbusho.
Gavana huyo akiendelea kuzungumza huku Naibu Spika akiendelea kutafsiri. Kulia ni msaidizi wa Gavana huyo, Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa Nigeria.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Fund na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akitoa hotuba yake na kushukuru ugeni huo.
Wakielekezana jambo. Kulia ni Tijan Babangida aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Nigeria, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Gavana huyo....
Wakisalimiana na viongozi baada ya kuwasili Shule ya Msingi Makumbusho
Gavana akipozi kwa picha na mwanafunzi Abdul aliyemtangaza kuwa ni mwanawe kuanzia jana
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja....

No comments: