ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 31, 2018

MWANAMKE WA KITANZANIA AUWAWA KINYAMA UINGEREZA

MTANZANIA Leyla Mtumwa (36) mkazi wa Arusha aliyekuwa akiishi Uingereza anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake na mwanaume mwenye umri wa miaka 38 (jina halijatajwa) ambaye pia ni Mtanzania anayesemekana kuwa ni mpenzi wake waliokuwa wakiishi naye pamoja.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kamkia jana Machi 30, 2018, katika nyumba wanayoishi Watanzania hao iliyopo eneo la Haringey, Kirkstall Avenue, N17 jijini London, baada ya kuzuka ugomvi baina yao ikiwa ni muda mfupi baada Leyla kurejea nyumbani akitokea disco la usiku alikokuwa amekwenda na marafiki zake.

Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa, alirudi kutoka disco akiwa na rafiki yake wamelewa na kuingia ndani, ambapo alimkuta mpenzi wake ambaye alianza kufoka na kutukana jambo lililoibua mzozo mkali baina yao.

Baada ya mzozo huo kuwa mkubwa rafiki aliondoka na ndipo jamaa huyo alianza kumshushia kipigo kisha kumchoma visu mbele ya mtoto wake wa miaka 12, ambaye Leyla alizaa na mumewe wa kwanza anayedaiwa kuwa ni raia wa Nigeria.

Ikiwa ni majira ya saa 1:00 asubuhi, hali ya Leyla ilikuwa mbaya, kijana huyo alipiga simu katika kitengo maalum cha polisi cha makosa ya jinai (Met’s Homicide and Major Crime Command), kuwajulisha tukio hilo.

Baada ya polisi kuwasili walimkuta Leyla akiugulia majeraha ya visu huku akilia maumivu makali aliyokuwa akiyapata, walimchukua kwa Ambulance na kumpeleka hospitali.

Licha ya jitihada za polisi kuwahi, lakini Leyla aliaga dunia majira ya saa 2:11 asubuhi kwa saa za London. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakimshikilia mwanaume huyo wa Leylakama mtuhumiwa namba moja wa tukio hilo.

Stori na GPL

2 comments: