ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 31, 2018

TANZIA UK NA TANZANIA

Ndugu wanafamilia kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa ya kifo cha mtanzania mwenzetu *Bi.Leyla Mtumwa kilichotokea tarehe 30 March 2018 jijini London kwa kuchomwa kisu na mumewe na kufariki papo hapo.*

Mwili wa marehemu bado unahifadhiwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi na taratibu nyingine,tutaendelea kupeana taarifa zaidi jinsi zitakapokuwa zinatufikia.

*Kwa niaba ya wanajumuia na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na Ireland kaskazini tunatoa salamu za rambirambi na pole kwa Ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu*

Tunawaomba wanajumuia na Watanzania wenzetu wote UK, NI, IRELAND na popote katika Diaspora ya Watanzania ulimwenguni , pamoja na kuwafariji familia tunatoa rai ya michango ya hiari ili kufanikisha gharama za kusafirisha Mwili wa Marehemu na gharama nyingine kwenda Nyumbani ARUSHA Tanzania

Anuani ya eneo la msiba hapa UK ni:

*39 Handsworth Road*
*Postcode N17 6BD*
*TOTTENHAM*

Unakaribishwa kufanya hivyo na kutoa rambirambi zako kupitia

*Akaunti ya Jumuiya.*

*A/c Name: Tanzania Diaspora in the UK*

*Sort Code: *30 - 99 - 08*

*Account No. *21906460*

*International*

*BIC: LOYDGB 21244*

*IBAN: GB74 LOYD 3099 0821 9064 60*

Tafadhali weka reference *"Leyla Funeral*”

Fedha hizi zitawakilishwa kwa familia ya Marehemu Kama sehemu ya mchango wa kufanikisha Safari ya mwisho ya mwenzetu.

Tunawaomba tuendelee kuwafariji na kuwaombea wenzetu wanapopita katika kipindi hiki kigumu cha Majonzi.

*R.I.P Leyla Mtumwa*

*UONGOZI*

*Jumuiya ya Watanzania UK & NORTHERN IRELAND*

*TZUK DIASPORA*

*Copy and Paste weka jina lako na kiasi unachochanga kwa hiari*

1. Abraham Sangiwa.  £50✅

2. Maryam Seif.            £30✅

No comments: