ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 30, 2018

Wabunge sita wapata ajali Morogoro, kuletwa Dar kwa matibabu

Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya  

Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali ya gari jana usiku Machi 29, 2018 mkoani Morogoro wakati wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Baada ya kutokea ajali hiyo saa 2 usiku katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Bwawani, wabunge hao waliumia maeneo mbalimbali ya miili yao na kukimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Wabunge hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).
Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya amesema majeruhi hao walipokelewa saa 3 usiku na kupatiwa huduma za awali.
"Jana tumepokea majeruhi sita walioumia sehemu mbalimbali na mmoja wao alilazimika kulazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) lakini hali yake inaendelea vizuri,” amesema.
“Leo asubuhi tayari tumewapa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi zaidi.”
Dk Rita amesema Kimbe na May ndio wameumia zaidi, kupata maumivu makali.
Taarifa zilizoifikia zinaeleza kuwa wabunge hao wanasafirishwa kwa ndege hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Chanzo: Mwananchi

No comments: