ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 30, 2018

WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAMEKUFA KWA KULA UYOGA WENYE SUMU

Watu watatu wa familia moja wakazi wa kata ya Sitalike katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamekufa baada ya kula uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu na wengine wawili wamenusurika kifo baada ya kupata matibabu katika hospitali ya manispaa ya Mpanda.

Bwana George Mrisho ni baba wa familia iliyokumbwa na msiba huo uliotokea Jumatatu ya tarehe 26 mwezi huu anaeleza kuwa waliofariki ni pamoja na mke wake mtoto na mdogo wa mke wake. 

Mganga mkuu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dokta Theopista Elias amethibitisha kupokea watu hao wanaodaiwa kula uyoga.



Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya Sitalike Bwana Adam Chalamila ametoa wito kwa wananchi wake kuwa makini na uyoga usiofahamika.

No comments: