ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 3, 2018

Ajali za barabarani zimeua 334 kwa siku 60



Waziri wa Mambo ya ndani Dk Mwigulu NchembaƂ 
By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz

Dodoma. Katika kipindi cha Januari hadi Februari 2018, zimetokea ajali 769 zilizosababisha vifo 334 na majeruhi 698, Bunge limeelezwa leo.

Akizungumza bungeni leo Aprili 3, Waziri wa Mambo ya ndani Dk Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi cha 2016 hadi 2018, jumla ya wahanga wa ajali 1,583 walilipwa fidia ya jumla ya Sh7.35 bilioni kutoka kampuni mbalimbali za bima.

Alikuwa akijibu swali la Rose Tweve (Viti Maalum-CCM) ambaye alitaka kujua katika kipindi cha 2016-2018 ni ajali ngapi zilizosababisha vifo na majeruhi.

Mbunge huyo ametaka kujua pia ni waathirika wangapi waliomba fidia na kulipwa.

Waziri amesema katika kipindi cha 2016/18 ajali zimepungua kwa asilimia 43 baada ya kutolewa elimu.

Amesema kuwa 2016 kulikuwa na ajali 9,856 zilizosababisha vifo 3256 na majeruhi 2128. Mwaka 2017 ajali zilikuwa 5310, vifo 2533 na majeruhi walikuwa 5,355.


No comments: