ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 3, 2018

Nape aitaka Serikali kutenga fedha ujenzi wa uwanja wa ndege Lindi

Waziri wa Tamisemi, Selemani Jaffo akimweleza
By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameiomba serikali kutenga fedha za ndani kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Lindi.

Akizungumza bungeni leo Aprili 3 katika kipindi cha maswali na majibu, Nnauye amehoji ni kwa nini uwanja huo usijengwe haraka na kwa kutumia fedha za ndani kwani ni uwanja wa kimkakati.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Joseph Kwandikwa amesema uwanja huo umetengewa fedha za ndani lakini akasema kwa sasa ni mapema kutaja kiasi.

Kwandikwa amesema katika bajeti ya mwaka huu kimetengwa kiasi kikubwa kwani serikali inatambua umuhimu wa uwanja, hivyo akamuomba muuliza swali asubiri wakati wa bajeti.

No comments: