ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 17, 2018

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA KAMANDA WA MATUKIO BLOG 
 Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.
 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
 Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi
maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.
 Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake.
Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya watu.
 Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo
la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Diwani wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.
 Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa
serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.
 Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha
maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.
 Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja
 la Ulongoni A.

 Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati  baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja  la Ulongoni A.
Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A

No comments: