ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 17, 2018

LEO NI SIKU YA MATEKA WA KIPALESTINA, 17 APRIL

 April 17 kila mwaka inakwenda sambamba na Siku ya Mateka wa Kipalestina, ambapo zaidi ya mateka elfu sita (6,000) wa kipalestina wapo katika magereza ya kivamizi ya Israeli.
Taasisi inayoshughulikia mambo ya mateka ya kipalestina,imetilia mkazo  ya kwamba historia ya harakati za mateka wa kipalestina,zimeanza mwanzoni mwa uvamizi wa Israeli katika ardhi ya Palesttina mnamo mwaka 1948 na kwamba utawala huo wa kivamizi wa Israeli umeifanya hatua ya kuwakamata watu ndio sera,njia na chombo cha kuwakandamiza na kuwadhibiti wananchi wa Palestina,pia kueneza woga na hofu kwa wapalestina hao.

Hali iliyopelekea ukamataji huo, kuwa sehemu ya msingi na thabiti ya sera yake katika kushughulika na Wapalestina na limekuwa ni jambo linalokera kila siku,pia kuwa ndio njia ya adhabu ya pamoja,kwani haipiti siku isipokuwa kunaripotiwa kesi za kukamatwa kwa wapalestina, huku ikikadiriwa idadi ya kesi za ukamataji katika miaka yote ya uvamizi kufikia zaidi ya kesi milioni moja. 

Tayari idadi ya mateka na waliokamatwa waliopo katika magereza ya kivamizi ya Israeli imefikia (6,500), miongoni mwao wapo watoto (350), mateka wanawake (62) wakiwemo kina mama (21), (8 ) wasiofikia umri wa kubaleghe , wabunge (6), (500)waliokamatwa bila ya tuhuma, wagonjwa (1800) wakiwemo (700) wanaohitaji uangalizi wa haraka wa kimatibabu, waandishi wa habari (19.

 Aidha mateka wengine (48) wamekamatwa tokea zaidi ya miaka ishirini na kuendelea, wengine (25) wamekamatwa tokea robo karne iliyopita, wengine (12) wamekamatwa tokea zaidi ya miaka thelathini iliyopita, huku wengine (29) wakiwa miongoni mwa mateka wa zamani zaidi waliokamatwa tokea kabla ya Mkataba wa Oslo, ambao  walipaswa kuachwa huru katika awamu ya nne mwezi Machi 2014, isipokuwa utawala wa Israeli ulikataa makubaliano hayo na kuwaweka mateka katika magereza yake.



Aidha,wameuawa zaidi ya 214 katika wanataasisi ya mateka tangu mwaka 1967 hadi April 8: (72) wameuawa kwa kuadhibiwa wakiwa mikononi mwa wachunguzi katika vituo vya uchunguzi huo, (60) wameuawa kwa sababu ya kutopewa matibabu, (7) wameuawa kwa kukandamizwa na kupigwa risasi na wanajeshi walinzi, (75) wameuawa ikiwa ni matokeo ya mauaji ya makusudi,mpango wa kivamizi kusafisha  ili wasiwepo wapalestina na mauaji ya moja kwa moja baada ya kuwakamata.  Matukio na mashuhuda wanaonesha kuwa,idadi kubwa ya waliopita kizuizini au kukamatwa,wamekumbana na aina mojawapo ya mateso ya kimwili,kinafsi,unyanyasaji wa kisaikoloji,mateso mbele ya halaiki au familia.


Katika kuilenga taasisi ya mateka na kuibana,bunge la Israeli (Knesset) likapitisha sheria nyingi za kibaguzi, zikiwemo sheria ya kuwaadhibu mateka wanaogoma kula ya mwaka 2015, ambayo inaruhusu kulishwa kwa sindano kama “drip”, sheria kali ya anaetupa jiwe,ikiilazimisha mahakama kumuhukumu kwenda jela kati ya miaka miwili hadi minne, huku likithibitisha usomaji wa kwanza wa muswada wa sheria unaoruhusu kulazimisha adhabu ya kifungo kwa watoto wa kipalestina chini ya umri wa (miaka 14), mbali ya miswada mingine ya sheria za hatari, kama vile rasimu ya sheria ya kuwaua mateka, kuwanyima elimu na mawasiliano, rasimu ya sheria ya ugaidi,adhabu kali kwa wahariri wa mpango wa Shalit na matumizi ya sheria ya jinai kwa wafungwa wanausalama.
Baraza la Taifa la Palestina kwa kuzingatia ndio mamlaka kuu ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina, mwaka 1974 wakati wa kikao cha kawaida kinachofanyika Aprili 17 ya kila mwaka, limepitisha kuwa siku hii ni siku ya kitaifa ya kuwaheshimu mateka na kujitoa kwao muhanga, kuwasaidia na kuunga mkono haki yao ya kuwa huru, pia kusimama karibu nao na wapendwa wao,vile vile ni siku ya kuwaenzi mashahidi wa taasisi za kitaifa zinazoshughulikia mateka.

No comments: