Advertisements

Sunday, April 29, 2018

SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasili katika Viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la OSHA wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.

Na.MWANDISHI WETU


Serikali imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa.

Waziri alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto.

“Tuendelee kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri

Waziri aliongezea kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa na mazingira salama , Lazima kuwe na mikakati ya pamoja baina ya utatu katika masuala ya kazi na ajira ikiwemo na kujenga utamaduni wa kujikinga na vihatarishi sehemu za kazi vinavyoweza kusababisha kuhatarisha afya na usalama wa wafanyakazi.

Aidha kama Taifa lazima tuoneshe umuhimu wa kuhakikisha kampeni hii inakuwa na matokeo chanya na kuendelea kuwa na Taifa lenye maendeleo.

Waziri aliongezea kuwa kulingana na Matokeo ya Utafiti wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliofanyika mwaka 2014 na matokeo yake kuchapishwa mwaka 2016 ulibainisha kuwa, hali ya ajira hatarishi za watoto kuzidi kuwa mbaya zaidi katika sehemu za mashambani, sekta ya madini, misitu na uvuvi.

“Kwa mujibu wa taarifa za Mtakwimu Mkuu wa Serikali za mwaka 2014 zilibaini kuwa watoto wenye umri kati ya miaka 5-17 walioko kwenye ajira ni takribani milioni 4.2 ambayo ni asilimia 28.8 ya wafanyakazi wote na kati ya hao asilimia 21.5 wako kwenye ajira hatarishi hususan sehemu za mashambani ambako asilimia 35.6 ya wafanyakazi wote ni watoto”,alisisitiza Mhe.Waziri

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alieleza kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa bila kukiukwa hususan kwa makundi maalum iliwemo yale ya vijana na makundi ya watu wenye ulemavu.

“kwa kuwa Vijana wadogo ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo wanastahiri kulindwa na kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuwa na kizazi endelevu,”alisema Mwenda

AWALI

Aprili 28 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya kuadhimisha masuala ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi, ambapo huwa na Kauli Mbiu inayotumika duniani kote ambayo inatolewa na Shirika la Kazi la Duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kizazi Salama chenye Afya –Generation Safe and Health”.Kaulimbiu hiyo ili kuendana na mazingira ya nchi yetu iliboreshwa na kuwa “Kizazi Salama Chenye Afya kwa Uchumi wa Viwanda –Generation Safe and Health for Industrial Economy”.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mzee Juma Nyinge aliyetembelea katika mabanda ya maonesho wakati wa Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018.
Afisa Mahusiano na jamii kutoka Kampuni ya Acacia Bi. Agripina Joseph akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiuliza swali kwa Afisa Usalama kazini Bw. Mlewa Mustapha kutoka Mgodi wa Buzwagi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea zawadi kutoka kwa Kampuni ya Acacia waliposhiriki katika maonesho ya kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.
Mwalimu wa wasioona Steven Changalo akiandika jina la mhe.Waziri Mhagama kwa kutumia vifaa wezeshi alipotembelea banda la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu.
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda akizungumza jambo wakati wa Kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyoadhimishwa mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu akitoa salamu kwa washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa vyeti kwa washindi wa maonesho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi na washiriki waliohudhuria wakati Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA pamoja na watendaji wa Idara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments: