Advertisements

Saturday, May 5, 2018

MAREKANI YATOA FEDHA ZAIDI KUPAMBANANA UKIMWI TANZANIA

Kaimu Balozi wa Marekani, Dk. Inmi Patterson akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana ambapo Serikali ya Marekani, kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR), umetangaza fedha zaidi Dola Milioni 512 (takribani Shilingi Trilioni 1.17) kupambana na janga la VVU/Ukimwi nchini Tanzania. (Picha: Kwa Hisani ya Ubalozi wa Marekani).
The ChargĂ© d’Affaires of the United States Embassy, Dr. Inmi Patterson and the Deputy Minister for Health, Dr. Faustine Ndugulile address the media during at the Mnazi Mmoja Hospital in Dar es Salaam yesterday where the US government, through the President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), announced an additional $512 million (approximately 1.17 trillion TZS) to combat the HIV/AIDS epidemic in Tanzania. (Photo: Courtesy of the US Embassy).

Ubalozi wa Marekani
 Dar es Salaam
TANZANIA
Mei 4, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Marekani yaahidi tena kupambana na VVU/Ukimwi nchini Tanzania


Dar es Salaam, TANZANIA. Ijumaa hii, Mei 4, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson ametangaza wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam akiwa na Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile, kwamba Serikali ya Marekani, kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR), umeahidi fedha zaidi Dola Milioni 512 (takribani Shilingi Trilioni 1.17) kupambana na janga la VVU/Ukimwi nchini Tanzania. Ukiwa umeandaliwa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania, Mpango wa PEPFAR nchini unalenga kudhibiti janga la VVU/Ukimwi ifikapo Septemba 2019.  Serikali ya Marekani, kupitia PEPFAR, imetumia zaidi ya Dola Bilioni 4.5(takribani Shilingi Trilioni10.26) kuzuia maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini toka 2004.


“Ninayo furaha kutangaza leo kwamba kupitia PEPFAR, Serikali ya Marekani itatumia fedha zaidi Dola Milioni 512 (takribani Shilingi Trilioni 1.17) kuboresha kinga ya VVU, upimaji na tiba nchini Tanzania hadi Septemba 2019. Matokeo kutoka Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi Tanzania ya Desemba 2017 yametuonyesha kwamba Tanzania iko nyuma ya nchi nyingine za kikanda. Mathalan, ni karibu nusu tu ya waathirika wa VVU nchini waliopimwa na kujua kwamba wana VVU. Tanzania inabidi irudi katika mstari na hii itahitaji juhudi kubwa katika uelimishaji umma na watu kupimwa, juhudi za haraka kuendana na sera mpya, na utekelezaji wa haraka wa sera hizo.”

PEPFAR inahamasisha kila mtu, hususan wanaume, kuongea na wafanyakazi wa afya kuhusu kupimwa VVU. Mtu yeyote anayegundulika kuathirika na VVU anaweza kuanza matibabu mara moja. Takribani Watanzania milioni moja walioathirika na VVU wako katika tiba ya kuokoa maisha, na wengi wao wanaishi maisha marefu na ya afya na wana viwango vya chini vya virusi kiasi kwamba hawawezi kuwaambukiza wengine, wakiwemo wenza wao na watoto.

Kwa taarifa zaidi kuhusu PEPFAR nchini Tanzania tafadhali tembelea tovuti ya Ubalozi wa Marekani: https://tz.usembassy.gov/our-relationship/pepfar/.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu hii taarifa, tafadhali piga simu Ubalozi wa Marekani Ofisi ya Habari Simu: +255 22 229-4000 au baruapepe: DPO@state.gov.

Usuli kuhusu Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) nchini Tanzania

Usuli wa mpango na takwimu za matokeo ya mpango:
           Katika mwaka wa fedha2017 pekee, PEPFAR iliweza kupima VVU kwa Watanzania milioni 9.
           PEPFAR inahudumia Watanzania 950,000 walio katika tiba ya kuokoa maisha yao (antiretroviral treatment); Lengo: Watanzania milioni moja kuwa katika tiba ya kuokoa maisha yao ifikapo mwisho wa 2018
           Katika mwaka wa fedha 2017, PEPFAR iliweza kutoa tiba ya kuokoa maisha kwa akina mama wajawazito 56,000 ili kuzuia maambukizi ya VVU kati ya mama na mtoto.


Tangu PEPFAR ilipoanzishwa mwaka 2003:
           Vifo vinavyohusiana na Ukikwi vilipungua kwa asilimia70, kutoka 110,000 mwaka 2003 hadi 33,000 mwaka 2016
           Maambukizi mapya kwa mwaka  yameshuka kwa karibu nusu kutoka 100,000 mwaka 2003 hadi 55,000 mwaka 2016
           Mpiango ya VVU Tanzania ilizuia maambukizi mapya milioni 1.1 na vifo  690,000


Ahadi ya PEPFAR ya miaka 15 kwa Watanzania inaashiria thamani ya mahusiano ya muda mrefu kwa watu wa Tanzania:
           Kupitia PEPFAR, Serikali ya Marekani imetumia takribani Shilingi Trilioni  9  (Dola Bilioni 4 )
           Fedha kwa mwaka 2018 ni zaidi ya Shilingi Trilioni1 (Dola Milioni 512)
           PEPFAR kwa sasa inatoa asilimia 73.8 ya fedha kwa ajili ya miradi ya VVU nchini Tanzania
           PEPFAR inatoa asilimia 68.0 ya fedha kwa ajili ya dawa za kufubaza (ARVs) na asilimia 81.3 ya fedha kwa ajili ya vipimo vya haraka.

No comments: