Advertisements

Friday, May 4, 2018

TASWIRA MUBASHARA YA TANZANIA DAY DALLAS MAMBO YALIKUWA HIVI HAPA CHINI NDIYO HABARI YENYEWE

Tanzania Day Dallas 2018 mambo yalikuwa mubashara kabisa watu walipata nafasi ya kujionea mambo mengi yanayo fanywa na Watanzania waishio Tanzania na wa ughaibuni. Lakini zaidi ya yote kivutio kikubwa kilikuwa kwa mzee John Stephen Akhwari, Mzee Akhwari ni mkimbia mbio ndefu wa miaka ya 60  ni Mtanzania alieacha history pale alivyomaliza mbio ndefu za Olympics za mwaka 1968 huko Mexico akiwa ameumia mguu na kugoma kupewa huduma ya kwanza na kukataa kubebwa na gari la wagonjwa hadi amalize mbio kwanza na kusema  ya kuwa akutumwa na nchi yake ya Tanzania kwenda kuanza mbio alitumwa kwenda kumaliza usemi ambao dunia unautambuwa na kuuheshimu hadi umekuwa ujumbe kwa kutia moyo kwenye maisha ya hapa duniani. Mzee Akhwari alialikwa  Dallas , TX kutoka Tanzania na kupewa tunzo ya heshima kwa kuwa mtu muhimu sana kwenye nyanja ya mchezo wa mbio ndefu  Tanzania na Duniani. Hapo juu video ya mzee John akifanya yake huko Mexico.
Hapa ni Mzee John Stephen akiwa na mvinyo wake kiroho safi, Taswira mzima ya jinsi mambo yalivyokuwa yamebamba kuanzia ijumaa, jumamosi, jumapili mambo ya ukodak wa kwenye zuria jekundu.

Mambo ya mduara na vidole juu.


Mambo ya Okodak wa kwenye zuria mambo zaidi jitirirshe kwa kwenda soma zaidi


 
   

No comments: