Advertisements

Friday, June 8, 2018

Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida Waendelea Kunolewa Namna ya Kutumia Mfumo Mpya wa Malipo Epicor 10.2.

Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mfumo huo kwa Wahasibu wa Manispaa ya Singida, leo Jijini Dodoma.
Mkufunzi wa mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Augustino Manda (aliyesimama) akiwaelekeza Wahasibu wa Halmashauri ya Iramba maeneo yaliyoboreshwa katika mfumo huo mpya wa malipo, leo Jijini Dodoma
Watumishi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sector za Umma (Ps3) Bw. Majiga Robert (wa kushoto) na Jimmy Mungai (wa kulia) wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa malipo Epicor toleo Na. 10.2 yaliyoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na PS3, leo Jijini Dodoma.
Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Dodoma na Singida wakijengewa uwezo namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo ulioboresha (Epicor 10.2) unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serika za Mitaa hapa nchini.
Afisa Msimamizi Fedha Mkoa wa Dodoma, Bw. Elisius Gujenji (aliyesimama) akiwaelekeza jambo juu ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) Wahasibu wa Halmashauri ya Chamwino, leo Jijini Dodoma. 

(Picha Na; Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.)



No comments: