Advertisements

Wednesday, July 4, 2018

KAZI KIPENGA KUCHUKUA DIMBA LA KATI MTANANGE WA SIMBA NA YANGA WASHINGTON, DC

Kazi Kipenga akimtoa nje ya uwanja mchekeshaji Joti siku ya mechi ya timu Kiba na timu Samatta uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Tanzania.

Kazi Kipenga Refa aliyechezesha mechi ya timu Kiba na Timu Samatta ndiye atakayechezesha mpambano wa Simba na Yanga Washington, DC
July 7, 2018 kuanzia 4pm kabla ya mpambano huo kutakua na sherehe za Simba Day zikitanguliwa na Bonanza la mpira wa kikapu litakaloanza 10 am.
Siku hiyo patakua hapatoshi kama wewe ni shabiki wa Simba pendeza kimavazi nyekundu na nyeupe tukuone, kama wewe ni shabiki wa Yanga vunja kabaki kwa njano na kijani anuani ya uwanja ni 830 Ridge Rd, SE,
Washington, D.C. 20019

KARIBU tufurahi pamoja kumbuka hii ni OLD SCHOOL REUNION LIKE NEVER B4 nunua tkt mapema kuondoa usumbufu.

No comments: