Advertisements

Tuesday, July 3, 2018

Mbunge Majimarefu afariki dunia

Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM),  Steven Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu amefariki dunia  usiku wa Julai 2,  2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 
Taarifa ya kifo cha mbunge huyo imethibitishwa na ofisa uhusiano wa Muhimbili,  Aminiel Eligaeshi.
 
Juni 20,  2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu. Hata hivyo kilichokuwa kikimsumbua mbunge huyo hakikuwekwa wazi.
 
Juni 6,  2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe,  Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu MNH

No comments: