Advertisements

Saturday, July 14, 2018

Monalisa, Mama Bishanga washiriki African Film Festival 2018 Dallas Texas USA

                                                                 Kelechi Eke                              Mama Bishanga
                    E:\PHOTO-2018-07-08-16-44-46.jpg                                                                        
   Andy Buyo Producer. Nigeria Mashebelele South Africa Film camera men
                    E:\PHOTO-2018-07-08-16-40-06.jpg
Mama Bishanga, Monalisa , Itika Jane Tanzania, na Gerry Mafokeng South Africa
Tamasha la filamu kwa nchi za Africa lilifanyika Dallas Texas, Amerika tarehe 03/07/2018. Nchi mbalimbali za Africa zilishiriki pamoja na South Africa ambayo Mzee Gerry Mafokeng aliecheza filamu maarufu miaka ya 2005 ya Totsi alishiriki na kupata award. Kenya, Nigeria, Zambia, Mozambiki, Uganda, Central Africa na Tanzania nchi yetu alishiriki Monalisa, na mimi nilipata mwaliko maalum, pia   walikuwepo wa Tz wanaoishi hapo Dallas Itika na Jane na wengine waliotoka state mbalimbali. Hii ilikuwa nafasi nzuri kujifunza mengi hasa ukizingatia Tanzania ilishiriki nafasi moja tu ya documentary ya Zanzibar wakati nchi zingine zilishiriki vipengele vingi na kupata award hata zaidi ya tatu. Monalisa anarudi nyumbani Tz na maelezo ya kutosha kufanikisha wasanii wa fani ya filamu kushirki mashindano ya mwakani.
Tamasha liliandaliwa na Kelechi Eke, Director wa kampuni yake Bigobi Production. Kelechi pia in Actor na Writer. Kelechi ni Mnigeria anayeishi Dallas Texas ambaye anajishughulisha na kutengeneza filamu za kiafrika akishirikisha wasanii wa Nigeria pia nchi zingine za Africa ikimwemo Tanzania, ambapo Itika Michael ni mmoja wa watanzania waliowahi kushirki filamu za Bilogi Production Company. Hongera Kwa Director Kalechi Eke
Hizi ni nafasi muhimu kwa wasanii kupata nafasi ya kushiriki na kujifunza mengi nje ya nchi yetu, pia ni nafasi ya kuona upande mwingine wa dunia. Tafadhali jitokezeni kushiriki tamasha hili ambalo hufanywa kila mwaka, kati kati ya mwaka, tumieni hii nafasi kupata msaada na maelekezo zaidi kwa Monalisa ambaye alipata award ya heshima. Hongera sana Monalisa .

Mwisho: Ombi langu kwa Waziri wetu Mwakyembe kutoa msaada wa kila aina kwa wasanii hasa wa kitaalamu kuandaa productions, documentary na mengineyo kukamilisha kazi zitazowasilishwa kushindana.

No comments: