ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 12, 2018

ABDI KASSIM BABI: CANNARO KUSTAAFU NI SAWA MAANA ANGEKECHESHA SANA KWENY...


Kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Abdi Kassim Babi ‘Ballack wa Unguja’ amesema Cannavaro amefanya maamuzi ya kustaafu kwa wakati sahihi vinginevyo angechekesha uwanjani.

Kama hujui basi mchongo upo hivi, Cannavaro na Babi walikuwa wanakaa chumba kimoja wanapokuwa kambini wakiwa Yanga, Taifa Stars na Zanzibar Heroes. Ni watu walioshibana na wanaofahamiana vyema.

Kubwa kabisa, Babi ndio alimkabidhi Cannavaro kitambaa cha unahodha kwenye mchezo wa Mapinduzi Cup mwaka 2010, Zanzibar. Tangu hapo Cannavaro amekuwa nahodha mkuu wa Yanga hadi anapotangaza kustaafu.

No comments: