Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche mara baada ya kuwasili Gereza la Wilaya Same kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia leo Julai 31, 2018, Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuendelea na ukaguzi katika magereza ya mwanga na Gereza Rombo. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche akitoa taarifa fupi ya Magereza Mkoa Kilimanjro kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kuongea na Maafisa na askari wa Gereza Same.
Maafisa na askari wa Gereza Same wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza(hayupo pichani) alipotembelea gerezani hapo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiongea na Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Wilayani Same(hawapo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa kwanza kushoto) akikagua nyumba ya askari inayojengwa kwa njia ya kujitolea katika Gereza la Wilaya ya Same. Nyumba hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia nne za askari hivyo kutatua uhaba wa nyumba katika gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo kwa lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo Mkoani Kilimanjaro leo Julai 31, 2018(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment