ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 21, 2018

WAZIRI KALEMANI AMUONDOA MENEJA WA TANESCO MEATU KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI

 Aliyekuwa Meneja wa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo Septemba 20, 2018.
  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
  Baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
 Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto)  akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
 Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi waWakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu, Septemba 20,2018.
 Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Medard Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonesha wananchi wa Kata ya Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA , alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae katika nafasi ya umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kumpangia kazi nyingine.

Waziri KALEMANI amechukua hatua hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu  akiwa katika ziara yake ya kukagua  kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba 20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa mradi wa umeme  katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.

Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya kutosha na vituo vya kutosha.

“Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika, pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”

“Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi, namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme hapa” alisema Dkt. Kalemani.

Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya  MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia wautumie kwa ajili ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu una asilimia sabini ya Mradi wa Umeme wa  REA ambapo wilaya ya Meatu  ilikuwa nyuma katika mradi huo ikilinganishwa na wilaya nyingine.

Aidha, amesema wananchi wa Meatu wakipata umeme utekelezaji wa Sera ya Viwanda utafanikiwa kwa kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha pamba Tanzania na ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha alizeti katika mkoa wa Simiyu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum  Khamis akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo hilo ameishukuru Serikali kwa kufanikisha utekelezaji wa usambazaji wa umeme katika vijiji vya wilaya hiyo na akaomba Wakandarasi waongeze kasi ili umeme awafikie wananchi kwa wakati


Naye mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Barnabas  Lupande ameahidi kuyafanyia kazi  maagizo ya  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyoyatoa katika kuakikisha kazi kusambaza umeme kwa wananchi inafanyika inavyotakiwa.

No comments: