Advertisements

Tuesday, October 23, 2018

KAMATI ZA BUNGE ZAFANYA VIKAO VYAO JIJINI DODOMA

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongoozwa na Mwenyekiti Mhe. Naghenjwa Kaboyoka wamekutana na Mwenyekiti wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  (TPA). 
 Viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana nao katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma Leo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndugu Deusdedit Kakoko na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Ignas Rubaratuka.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)  Mhe. Abdallah Chikota akizungumza katika kikao cha Kamati  hiyo kililchofanyika Jijini Dodoma leo ambapo walikutana na Halmashauri ya Kilwa.pembeni ni Katibu wa Kamati Ndugu Victor Mhagama.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Abdallah Chikota wamekutana na Halamshauri ya Wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Renatus Mchau akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Halmashauri hiyo ilipokutana na Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Kahama Ndugu Anderson Msumba wakati Kamati hiyo ilipokutana na Halmashauri ya Mji huo katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Vedasto Ngombale akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana  leo Mjini Dodoma, pembeni ni Katibu wa Kamati hiyo

No comments: