ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 26, 2018

KUFIKIA 2020 MAJI YATAKUWA YAMEFIKA VIJIJINI KWA ASILIMIA 85: MAKAMU WA RAIS SAMIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akigusa eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo kwenye mchoro huo wakati wa ziara yake mkoani Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza ahadi ya kusambaza maji mjini na vijijini ambapo mpaka ifikapo mwaka 2020 inategemea maji yatakuwa yamefika vijijini kwa asilimia 85% na mjini asilimia 90%.Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa tanki kubwa la mradi wa maji Bagamoyo lenye uwezo wa kubeba lita milioni 6 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku sita mkoani Pwani. Makamu wa Rais ameipongeza Dawasa kwa kazi nzuri na amewataka wananchi kupitia kamati mbali mbali za maji kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji, miundo mbinu pamoja na mazingira yake. “Wote tujitahidi kutunza vyanzo vya maji”alisema Makamu wa Rais Tenki hilo la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa mji wa Bagamoyo na vitongoji vyote vinavyozunguka mji huo.

Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kutembelea mradi wa uzalishaji na usambazaji vifaranga wa kampuni ya AKM Glitters na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo.Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na vIongozi wengine wa Chama na Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) juu ya miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) juu ya miundo mbinu ya maji itakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la maji litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kukagua Mradi wa tanki la maji wilayani Bagamoyo litakalokuwa na uwezo wa kubeba lita milioni 6, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu wakati wa ziara yake kwenye eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo mkoani Pwani

No comments: