ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 25, 2018

WAZIRI AWESO AELEKEZA TIMU YA WATALAAM WA MAJI WA WIZARA KUKAGUA MIRADI YA MAJI WILAYANI MBULU

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), watatu kushoto mstari wa mbele-meza kuu, akiwa katika moja ya mkutano wa hadhara wilayani Mbulu. Pichani ni katika uwanja wa kata wa Haydom.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Haydom wilayani Mbulu. Ameelekeza fedha za dharura kiasi cha shilingi milioni 60 zitumike kuchimba kisima cha maji katika mji wa Haydom.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), anayetizama kamera, akiwa katika mradi wa maji wa Mongahay – Tumati wilayani Mbulu, ameagiza wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji kukagua miradi yote ya maji wilayani Mbulu ili kubaini changamoto za kitaalam na kutoa ushauri kuhusu namna ya kukamilika kwa miradi hiyo mara moja ili huduma ya majisafi iwafikie wananchi kwa uhakika.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia upatikanaji majisafi na salama kwa wananchi katika kioski cha Kwa Zacharia mjini Hanang’. Hata hivyo, Waziri Aweso ameelekeza miradi ya maji ikaguliwe kwasababu kiwango chaupatikanaji maji wilayani Mbulu hakitoshi
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipewa maelezo kuhusu mradi wa maji wa Dongobesh kutoka kwa mtalaam wa maji wa wilaya ya Mbulu Onesmo Mwakasege.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akishiriki kazi ya kuchimba mtaro kupata nafasi ya kukarabati bomba linalosambaza maji kwa wananchi katika mtaa wa Stendi ya zamani, mjini Haydom Mbulu.

No comments: