ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 24, 2018

Zimamoto watoa Elimu ya Uokozi kwa Abiria Stendi ya Ubungo

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Temeke, Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, akitoa Elimu ya Uokozi kwa abiria katika Stendi ya Ubungo wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali nchini katika kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.Jeshi hilo linatoa elimu hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza safarini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limeanza kutoa elimu ya Uokozi kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wa kupunguza majanga pindi inapotokea dharura pale vyombo vya usafiri vinapopata matatizo njiani.

Akitoa elimu hiyo katika mabasi mbalimbali Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Temeke, Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, alisema jeshi limejipanga kutoa elimu katika stendi za mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya abiria wengi kutoelewa elimu ya uokoaji pindi yanapotokea majanga njiani.

“Tunahudumia Watanzania na tunapenda kuona wananchi wanaenda kushuerehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka  na wanarejea katika maeneo yao salama,na sisi kama jeshi tutahakikisha askari wetu wanakuwepo kazini masaa ishirini na nne ili watoe msaada pale utakapohitajika” alisema Kamanda Puyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti abiria wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali nchini wamesema wanashukuru kuona jeshi la zimamoto limejiongeza na hii  ndio inavyotakiwa kwani kumekua na majanga mengi njiani yanayosababisha watu kupoteza maisha.


“Hatukua na elimu ya kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, tunarishukuru jeshi kwa kutoa elimu hiyo na tunaomba waendelee na utaratibu huo sio katika kipindi hiki cha sikukuu tu bali iwe programu endelevu” alisema Ayoub Mtekela.

No comments: