Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi jana Jumatano Agosti 7, 2019 aliwasimamisha kazi watumishi 183 wa wizara hiyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Watumishi hao ambao waziri huyo amekabidhi majina yao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya uchunguzi, wanadaiwa kuingilia mfumo wa kukadiria na kukusanya kodi ya pango ya ardhi kinyume na taratibu na kusababisha upotevu wa mapato ya Serikali.
Katika taarifa ya wizara hiyo, Lukuvi amemuelekeza katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha orodha ya majina hayo kwa mkurugenzi wa Takukuru leo na uchunguzi uanze mara moja.
Mwananchi limekuwekea orodha ya majina 183 ya watumishi hao, vyeo vyao na maeneo waliyokuwa wakifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment