ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 8, 2019

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI APATA KITABU KINACHOONESHA MADINI YAPATIKANAYO NCHINI.

Pichani Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Hassan Abbas akiwa katika Banda la GST na Mtaalam wa GST Mhandisi Priscuss Kaspana

 Tarehe Augusti 7, 2019 , Dr Hassan Abbas ambaye ni msemaji Mkuu wa serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania atembelea Banda la *GST* katika wiki ya Maonesho ya Mkutano Mkuu wa 39 wa *SADC* kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za kitaalam juu ya Madini na Miamba iliyopo nchini.

Kitabu hicho ambacho ni toleo jipya kinachoonesha Madini kuanzia ngazi ya Wilaya , kata na Kijiji kimeainisha Zaidi ya madini 220.

Akiambatana na jopo la waandishi wa Habari , Dr.Hassan alipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mtaalam Mhandisi Priscuss Kaspana hususani katika sekta ya Madini ya viwanda yaani Industrial Minerals.

Sambamba na taarifa hizo Dr.Hassan kwa niaba ya serikali alipata zawadi ya kitabu Cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo jipya

No comments: