Akifunga maonyesho ya nne wiki ya viwanda ya SADC jijini Dar es Salaam jana, Dk. Shein alisema juhudi kubwa inayofanywa na viongozi wa nchi wanachama kuimarisha uzalishaji kwa viwanda vya ndani inatakiwa isipotee bure kwa kuunga mkono juhudi hizo. Alisema, inawezekana kabisa kukuza masoko na kuongeza ajira kwa kutumia bidhaa za ndani kwa sababu msisitizo mkubwa ni kuona waafrika wanapenda vya kwao bila kuwa tegemezi wa bidhaa za kimagharibi. “Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anaunga mkono utelekezaji wa maazimio yaliyopitshwa katika vikao vilivyofanyika pamoja na mikakati ya Serikali zetu zote ya kuendeleza viwanda kwa kununua na kuzipenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe,” alisema na kuongeza: “Vile vile, tujenge utamaduni wa kuwapenda na kuwatumia wataalamu wetu wa ndani na tuondokane na utegemezi wa wataalamu wa nje, sambamba na kujenga misingi imara ya kuendeleza teknolojia yetu wenyewe. “Kufanya hivyo, ni kutafsiri kivitendo ile dhamira ya nchi zetu kuunda umoja wa SADC kwa ajili ya kuongeza fursa ya masoko na ajira. Tutaweza kuongeza masoko na ajira ikiwa tunanunua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe vinavyoendeshwa na wataalamu wazalendo. “Kwa msingi huo, nasisitiza haja na umuhimu wa kuzingatia falsafa na hekima za Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar kwa kuzingatia maneno aliyoyasema kwamba “Tukuza kilicho chako hadi usahau cha mwenzako”. Wakati umefika wa kuhakiksha kwamba tunapenda kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe.” Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema anaamini maonesho hayo aliyoyafunga jana yamesaidia na yatakuwa na mchango mkubwa katika utekelezaji wa mipango na mikakati tuliyonayo ya kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa viwanda katika nchi zote 16 wanachama wa SADC. Taaluma, ujuzi na maarifa yaliyopatikana katika maadhimisho na maonesho haya itatumika katika kukuza ubunifu wa kuendeleza viwanda, utafutaji wa masoko pamoja na kukuza uhusiano baina ya wazalishaji, wanunuzi, wasafirishaji, na watumiaji bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyomo ndani ya nchi Wanachama wa Jumuiya hii.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la SADC Peter Varndell akizungumza wakati wa hitimisho la Maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika SADC lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC Octavian Mshiu wakati akifunga maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yaliyokuwa yakifanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na viwanja vya Karimjee jijini.
Meza kuu.
Katibu Mkuu wa SADC Mhe. Dr. Stergomena Tax, wakati wa ufungajin wa Maonesho ya Nne ya Wiki ya Maonesho ya Viwanda ya SADC leo Jijini Dar es Salaam.yaliofanyika katika ukumbi wa Juluis Nyerere. Vile vile, anaamini maonesho hayo yamepanua fursa ya ushirikiano kati ya wenye viwanda ndani ya nchi za SADC na wamiliki wa viwanda na watoa huduma mbali mbali wa mataifa mengine nje ya umoja wa SADC. Hata hivyo, alishauri wazalishaji katika nchi wanachama ikiwa wanataaka kuingia kwenye ushindani watalazimika waongeze ubora wa bidhaa za viwandani, ili ziweze kushindana na zile ambazo watu wengine hupenda kuzinunua. Ubora katika utengenezaji na ubunifu wa hali ya juu utakaoweza kuwavutia wanunuzi wengi. Hali hii itaweka mazingira mazuri ya kupata masoko ya kutosha na ya uhakika pamoja na mitaji ya kujiendesha na kukuza ajira. “Naamini kwamba uwezo wa kufanya hivyo tunao, linalohitajika ni kushirikiana katika kuongeza ujuzi na bidii zaidi katika kazi zetu viwandani pamoja na kujiamini, kwamba tunaweza kuingia katika ushindani wa viwango na kuibuka washindi. Katika utafutaji wa masoko tuweke mkazo katika Technolojia ya Habari na Mawasiliano, ili tuweze kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokana na utandawazi,” alisema Dk. Shein. Akigusia kaulimbiu ya Maadhimisho na Maonesho ya SADC kwa mwaka huu wa 2019 ambayo imeweka msisitizo katika uwekaji wa mazingira mazuri kwa maendeleo ya viwanda, ili ilete manufaa mapana zaidi kwa jamii, alisema inakwenda sambamba na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zote mbili za kuimarisha viwanda. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuiimarisha sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha kwamba inaongeza fursa za ajira kwa vijana wetu wanaomaliza masomo yao katika ngazi zote. Serikali zote mbili zinaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kisera na za kimkakati katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kufikia hadhi ya nchi ya Uchumi wa Kati, kama ilivyoelezwa katika Mipango Mikuu ya Maendeleo ya Taifa.
Kaimu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe akizungumza wakati wa mkutano wa Ufungaji wa Wiki ya Nne ya Maonesho ya Viwanda ya SADC Jijini Dares Salaam.
Mawaziri wakitambulishwa...
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akitoa neno la Shukurani kwa Washiriki wa Wiki ya Viwanda kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, (hawapo pichani), Kuhusu maonesho ya Viwanda yaliyofungwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Wageni waalikwa.
Wageni wakifurahia.
Picha za pamoja za viongozi. Alisema, utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo Miradi ya umeme, barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege unalenga katika kujenga misingi imara ya ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara ambazo ni muhimu katika kutatua changamoto za ajira pamoja na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi. Katika hatua nyingine, Dk. Shein aligusia umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili katika nchi wanachama wa SADC ambapo alidai itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mtangamano kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika katika harakati za ukombozi. “Ni jambo jema kuona kwamba kuna wazo la kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa ni miongoni mwa lugha rasmi za mawasiliano katika majukwaa ya SADC. Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa Wanachama wa Jumuiya hii pamoja na kukuza shughuli za biashara na viwanda. “Historia inatuonesha kwamba Kiswahili kimeweza kuwaunganisha Watanzania kuwa wamoja, licha ya kwamba Watanzania wanazo lugha tofauti za makabila mbali mbali. Aidha, Kiswahili kimekuwa na mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Afrika. “Hivi sasa, Kiswahili kimerahisisha mawasiliano na kukuza biashara katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na tayari Umoja wa Afrika umekikubali Kiswahili kiwe ni Lugha rasmi. Kwa hivyo, wazo la kukifanya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha rasmi za SADC ni muhimu na vyema tukaungana katika kulifanyia kazi suala hili,” alisema Dk. Shein. Awali Katibu Mtendaji wa SADC, Dk. Stegomena Tax alisema maadhimisho hayo ya wiki ya nne ya viwanda yamekuja katika wakati muafaka ambapo Serikali ya Tanzania inaimarisha uchumi wa viwanda. Alisema, biashara ikikuzwa vema wananchi watapata faida na ajira pamoja na bidhaa zenye ubora ambazo zinazweza kuuzika hata nje ya mipaka ya nchi za SADC. “Ushiriki wenu katika wiki hii inamaanisha utayari mlio nao katika kukuza uchumi wa SADC, umuhimu wa kuzitambua fursa na kuhamasisha kuzichangamkia ni jambo la msingi katika ukombozi wa nchi za kiafrika kiuchumi, kijamii na kisiasa,” alisema Dk. Tax. Aidha, Dk. Tax alisisitiza umuhimu wa kuwepo mkakati madhubuti wa kuimarisha miundombinu ili kurahisisha usafirishaji bidhaa zitakazozalishwa kwenye viwanda vya nchi wanachama. Ambapo, wakati wa ufunguzi wa wiki hiyo ya viwanda Rais Dk. John Magufuli alisisitiza haja ya kuwa na miundombinu imara kwa kuunganisha nchi za SADC. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Innocent Bashungwa alisema zaidi ya washiriki 5352 kutoka nchi wanachama wamehudhuria wiki hiyo ya viwanda, huku waonyeshaji bidhaa 585 walionyesha bidhaa mbalimbali kutoka nhci wanachaa 14 za SADC. “Katika waonyeshaji hao kulikuwa na taasisi 61, viwanda 69, taasisi za fedha 65, Umoja wa Mataifa pia walishiriki na wajasiriamali 405. Huku watu waliotembelea maonyesho haya wanafikia 4767, hii ni ishara ya kukubalika na itasaidia kuongeza fursa kwa wazalishaji wa ndani kupata mtandao mkubvwa wa kuuza bidhaa zao,” alisema Bashungwa. Leo katika ratiba ya SADC washiriki kutoka nchi wanachama watatembelea viwanda mbalimbali nchini ili kuona namna bidhaa zinavyozalishwa na kutoa ushauri pamoja na kujifunza masuala mbalimbali katika sekta ya viwanda Tanzania Bara na Zanzibar. SADC inaundwa na nchi 16 ambazo ni Tanzania, Zambia, Malawi, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Eswatini, Botswana, Lesotho, Mauritius, Comoro, Ushelisheli, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Namibia na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment