Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu, Ndg. Ludovick Utouh alipowasili kwa ajili ya kufunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wajibu, Ndg. Ludovick Utouh kwa ajili ya kufunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Rais wa asasi zisizo za kiserikali, Ndg. Stigma Tenga na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wafanyakazi wa asasi zisizo za kiserikali wakati akifunga maonesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali 2019, kushiriki dhifa ya pamoja na ugawaji wa tuzo kwa asasi zilizofanya vizuri leo katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment