ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 26, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AJUMUIKA KATIKA CHAKULA MAALUM ALICHOWAANDALIA NA ASKARI WALIOSHIRIKI GWARIDE MAALUM LA MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA MAPINDUZI VIWANJA VYA ZIWANI POLISI ZANZIBAR.VIKOSI VYA ULINZI KUJUINA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar kuhudhuria hafla ya chakula Maalum alichowaandalia Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walivyoshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, lililofanyika 12, January 2020 katika viwanja vya Amaan,(kulia kwa Makamu ) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe.Zuberi Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar.Mhe. Omar Othman Makungu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Issa Haji Gavu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekjiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhi Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar kuhudhuria hafla ya chakula maalum alichowaandalia Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ, walioshiriki katika Gwaride Maalum la maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar lililofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 12, January 2020, hafla hiyo imefanyika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama na viongozi wa meza wakati ukipingwa wimbo wa Taifa alipowasili katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi. Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Bridegi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu)
MAOFISA wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakipiga saluti wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) katika hafla maalum ya chakula iliofanyika katika viwanja vya Polisi ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMZ na SMT walioshiriki katika gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa, katika hafla ya chakula Maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) katika viwanja vya Polisai Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MKUU wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, akizungumza wakati wa hafla Maalum ya chakula kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo picha) kwa Askari walioshiriki Gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar 12,January 2020.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ vilivyoshirika Gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar, 12,January 2020, katika chakula Maalum alichowaandalia katika viwanja vya Polisi ziwani Zanzibar (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seiuf Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ , wakijumuika katika chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya ziwani Polisi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa neno la shukrani kwa Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki katika Gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, lililofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar 12,January 2020. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ziwani Polisi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ , wakijumuika katika chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya ziwani Polisi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wac Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakiitikia dua ikisoma na Askari wa Kikosi cha FFU. Ndg.Issa Khamis Juma,(hayupo pichani) (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu)
ASKARI wa Kikosi cha FFU Issa Khamis Juma akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula Maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Askari walioshiriki Gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.lililofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.(Picha na IKULU)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mkuu wa Bridegi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula maalum alichowaandalia Askari Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan 12,January 2020, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Polisi Ziwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments: