ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 11, 2020

Kocha Mbelgiji Yanga aachwa kwenye mataa

By WAANDISHI WETU, Mwanaspoti
KOCHA wa Yanga, Luc Eymael akiwa na mkewe, Patricia wamejikuta akipokewa na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini leo mchana alipotua kutoka Ubelgiji

Tofauti na ilivyozoeleka kwa timu kutuma watu wa kuwapokea makocha au wachezaji wao wanapowasili nchini kutoka nje ya nchi, hali ilikuwa tofauti wakati Eymael alipotua kwani hakukuwa na mwakilishi wowote kutoka Yanga aliyejiokeza kumpokea.

Eymael ambaye ametua nchini leo saa 7;30 mchana na Shirika la ndege la Ethiopia, alijikuta akipewa usaidizi na waandishi mara baada ya kufanyiwa mahojiano ambao walilazimika kumtafutia usafiri wa kumpeleka nyumbani kwake, Masaki jijini.

Mbelgiji huyo alishtuka alipogundua kuwa hakuna mtu yeyote aliyetumwa kwa ajili ya kumpokea kwa kusema, "Inamaana nitembee kwenda nyumbani," huku kucheka.

Mwanahabari mmoja alionekana kumpa usaidizi Eymael kwa kuongea na madereva 'Tax' ambao walikuwa eneo hilo la uwanja wa ndege na kufikiana makubaliano ya bei kisha kocha huyo, akapanda na mkewe tayari kwa safari ya kupelekwa nyumbani kwake

Katika hatua nyingine, Eymael ameelezwa kushangazwa na taarifa zilizoenea hivi karibuni za kuongezeka uzito kwa baadhi ya wachezaji wake.

Alisema taarifa za kuongezeka kilo kwa wachezaji alizipata akiwa kwao lakini hata yeye zimemshangaza.

"Kuongezeka kilo inashangaza kiukweli kwa sababu tulitoa programu mbili kwa wachezaji ambapo kama wangezifanya vizuri basi wote miili yao ingekuwa sawa.

"Tatizo lingine kocha wa viungo anaweza akachelewa kuja kwa sababu mke wake anatarajia kujifungua hivi karibuni," alisema Eymael.

No comments: