Na Timothy Itembe Mara.
Wakuu wa shule za sekondari kutoka Mikoa ya kanda ya Ziwa wamemwagia sifa serikali awamu ya sita katika swala zima la kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuondoa uhaba uliopo.
“Tunapongeza Serikali awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya 10 ndani ya mkoa Mara jambo ambalo litaenda kuchochea uboreshaji wa elimu ya sekondari”alisema Afisa elimu Mkoa wa Mara Mwl Benjamini Oganga.
Akiongea jana kwenye kikao cha pamoja kilichowakutanisha wakuu wa shule za sekondari kutoka Mikoa ya kanda ya Ziwa ambacho kilikalia ukumbi wa chuo cha ualimu Tarime(TTC) alisema ujenzi wa vyumba vya madara utaenda kuchochea elimu ikiwemo na swala zima la kuwapunguzia makali ya michango wazazi na walezi.
Afisa huyo aliongeza kusema kuna haja walimu kujenga tabia ya nidhamu mashuleni katika kuhakikisha wanafuta swala la ufaulu wa alama 0 na 4 kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya kuingia kidato cha tano na sita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa wakuu wa Shule za Sekondari Kanda ya Ziwa TAHOSSA Mwl: Mohamed Kajeri amezitaja schangamoto mbalimbali zinazokabili shule za sekondari ikiwemo Ruzuku ndogo ya fedha za chakula kwa shule za Bweni nakuomba serikali kutatua changamoto hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Stadi Kanda ya Ziwa Hezbon Mwera amesema kuwa wakuu wa shule waendelee kuchukua taadhari ili wanafunzi waweze kupelekwa vyuo vinavyotambulika na serikali ambavyo vimesajiliwa.
Mwera aliongeza kuwa taasisi yake imekuja na mpango wa kuwajengea uwezo wanafunzi ambao hawakubahatika kuchaguliwa na kujiunga na masomo ya juu ambapo wanatoa kozi mbalimbali za ufundi stadi kuhamasisha utalii wa ndani,kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana na wakina mama,ufundi magari na umeme.
Mkurugenzi huyo alitoa nafasi kwa wakuu wa shule za sekondari pamoja na walimu wote kuchangamkia fursa ya kusoma bure kozi fupi ndani ya chuo cha taasisi ya Mwera Faundation.
"Natoa nafasi bure kabisa walimu wakuu na walimu wote njooni mkasome bure unachagua mwenyewe kozi unayotaka pia walimu wa kawaida wapewe barua ya utambulisho tutawapokea na watajifunza bure" alisema Mwera.

No comments:
Post a Comment