Na Timothy Itembe Mara.
KATIBU wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime mkoani Mara,Valentine Deogratius amewakumbusha wanachana na wagombea kuzingatia kanuni za uchaguzi.
“Mwaka huu tuna uchaguzi wa Chama na jumuia zake ndani ya chama chetu ili kuwachagua viongozi ngazi mbalimbali kwa mjibu wa kikatiba na mkurugenzi wa ogonaizesheni ni katibu wa chama kwa hali hiyo nawataka wanachana na wagombea kuzingatia kanuni zilizopo”alisema Deogratius.
Katibu huyo aliongeza kusema ibara ya 83 kipangele kidogo cha 3 kinamtaja katibu kuwa ni mkurugenzi wa uchaguzi ndani ya chama na pia anashugulika na vikao ndani ya chama pamoja na wanachama ikiwemo kusimamia utekelezaji wa maazimio ya vikao.
Katika uchaguzi uliopo katibu huyo alisema wamejipanga na wametoa hamasa kwa njia ya vipindi vya redio na mikutano mbalimbali,kwa hali hiyo hatarajii kuona uchaguzi unaenda vinginevyo.
Kwa upande mwingine katibu huyo aliwataka vijana watu wenye ulemavu na wanawake kuchangamkia fursa ya kuomba nafasi za uongozi ndani ya chama zinazogombewa lengo kuwapata viongozi wenye nia ya kukijenga chama na kuisimamia serikali.
Niwatake wale wanaohusika kuzingatia wajibu kila moja ikiwemo kuchukua na kurudisha fomu za kugombea kwa wakati kwa kuwa fomu zipo kila kata nyingi na za kutosha na kwa yule ambaye atakuwa na malalamiko ofisi ipo wazi aandike barua mapema ili kushugulikia tatizo.
Katibu huyo alimaliza kwa kusema kuwa hatarajii kuona kanuni za uchaguzi zinakiukwa kwa sababu taratibu za elimu zimetolewa vya kutosha na ikitokea kuna mtu mmoja amekiuka sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kufutiwa wanachama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa Mara,Jacobo Mangallaya aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombe ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza kuwa hawashirikishwi
Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama kufanya uchaguzi wa huru na haki ili kuwapata viongozi waliobora kwa lengo la kuwapata viongozi ambao watawatumikia wanachama pamoja na kuimarisha chama.
Mangallaya aliomba uchaguzi kufanyika kwa uwazi na bila kutumia rushwa na kuwa watakao gombea nafasi mbalimbali wawe huru kupata matokeo ya uchaguzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi watakao teuliwa.

No comments:
Post a Comment