ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 2, 2022

MAMALISHE WAPATIWA SEMINA YA UTUNZAJI WA FEDHA


Na, Paschal Malulu

Kutokana na kutokuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na kuongezeka kwa malalamiko ya kutopata mikopo kutoka serikalini Mama lishe wametakiwa kuweka Akiba pindi wanapofanya kazi ili kukidhi Mahitaji.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Wazazi Wilaya ya kahama wa chama cha mapinduzi (CCM) Hassan Haruna wakati akizungumza na Mama lishe katika ukumbi wa Ghamma Hotel kwenye semina ya Mama lishe programme iliyoandaliwa na Shirika la Kahama Hope Givers.

“Asiwadanganye mtu kuwa serikali inatoa ajira hicho kitu hakipo wadau kama hawa wanaisaidia serikali hivyo na sisi kama serikali tupongeza hatua hii ya wadau kujitokeza na kusaidia makundi yote”.

Naye Mwenyekiti wa Kahama Hope Givers, Simon Kassala amesema lengo la kuanzisha Mama Lishe Programme ni kumwezesha kila sekta na kumpatia elimu na fursa mbalimbali.

“Semina hii ni mwanzo tu zitakuja nyingi lengo letu ni kuhakikisha tunasaidia akinamama lishe kuwa na akaunti kwenye taasisi za kibenki ili kujikwamua kiuchumi kwani pesa mnayoingiza mmekuwa mkiiona ndogo kumbe ni kubwa sana ikitunzwa vizuri”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huheso Foundation na Huheso Fm, Juma Mwesigwa amewapongeza Mama lishe kwa ujasiri na uthubutu wa kujiajiri na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

No comments: