
Akizungumza kwenye Mjadala huo amesema kuna uoga wa mabadiliko kwenye safari ya Dijitali "Najua kuna uoga wa mabadiliko, na changamoto kubwa anayoona ni digitali imekuwa ikidhibitiwa kisiasa".
Vilevile akizungumza Mjadala mwingine kuhusu Mikakati na Mbinu za kupambana na ufuatiliaji wa kidijitali, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums amesema katika dunia ambayo Nchi haiweki Sheria ya Faragha, utu wa watu wake unaweza kuwa matatani.
Amesisitiza Utu katika ulimwengu wa kidijiti ni wa kupigania kwa nguvu zote, akisema JamiiForums kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali inaendesha mafunzo ya usalama wa kidijiti
Amesema "JamiiForums ni rafiki mkubwa wa Wanahabari na tunaahidi kufanya mafunzo haya kwa Waandishi wa Habari".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mwaka 2022 yanayobeba Kaulimbiu isemayo, "Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti" yatahusisha Wadau wa Tasnia Habari kutoka ndani na Nje ya Nchi.

No comments:
Post a Comment