Advertisements

Wednesday, June 26, 2024

KENYATTA AMPA ONYO KALI RUTO KUHUSU MAANDAMANO YA VIJANA



Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta aiomba Serikali kuwasikiliza Wananchi, ametoa wito wa Amani dhidi ya maandamano yaliyoleta maafa makubwa nchini Kenya, wakati huu amewaomba Serikali kuwasikiliza Wananchi waliowapigia Kura.

Viongozi wote walichaguliwa na Wananchi kwa ajili ya kuwasikiliza Wananchi sio chaguo bali ni wajibu uliowekwa katika misingi ya katiba yetu na misingi ya Kidemokrasia, Serikali haiitaji kutumia nguvu dhidi ya wakenya wanaotekeleza haki zao katika maandamano ya Amani.

Kenyatta ameyataja matukio ya Jumanne ambayo waandamanaji wanaopinga maswala ya Kodi kuingia Bungeni na kwenye taasisi mbalimbali kuwa ni uhaini na watachukuliwa hatua dhidi ya waandamanaji watakaojihusisha na ghasia.

Ikumbukwe watu sita wamefariki na huku zaidi ya 100 wakiwa wamejeruhiwa japokuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Vijana walihamasishana kupitia mitandao ya kijamii kutokama na Musuada unaoenda kuongeza Ushuru mpya licha ya kutetea haki za binadamu maafisa wa Polisi kwa kutumia Risasi, Kenyatta alipongeza jeshi hilo kwa juhudi wanazozifanya za kupunguza Ghasia hiyo ili kurejesha utulivu.

Maandamano mengine yanatarajiwa kufanywa siku ya Alhamisi ambapo Wabunge watakuwa wanapiga kula dhidi ya Muswada huo.

No comments: