Advertisements

Wednesday, June 26, 2024

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, ofisini kwake Mlimani Jijini Dodoma, Juni 26, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo Jumatano amefanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

Majaliwa anakutana na viongozi hao kukiwa tayari kuna mgomo wa kutofungua maduka ambao unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

Mpaka sasa maeneo ambayo wafanyabiashara wamefanya mgomo kwa kufunga maduka yao ni Kariakoo jijini Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa, Mtwara, Tunduma pamoja na Dodoma.

Wafanyabiashara hao wamefunga maduka kushinikiza kupunguziwa kodi ambazo zinatozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

No comments: