Advertisements

Wednesday, July 3, 2024

ZIARA YA RAIS WA MSUMBIJI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara ya Kiserikali ya Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya Afya baina ya Tanzania na Msumbiji Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024. Kulia ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akitia saini Hati hiyo kwa upande wa Tanzania na kushoto ni Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Msumbiji Mhe. Manuel José Gonçalves akitia saini kwa niaba ya Serikali.



No comments: