ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 6, 2026

DKT. KIJAJI: UTALII WA HALAL NI ZAO JIPYA LENYE FURSA ZA KUONGEZA IDADI YA WATALII NA PATO LA TAIFA *

 *


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), amesema kuwa Utalii wa Halal (Halal Tourism) ni fursa mpya itakayoongeza idadi ya watalii  na pato la Taifa.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo leo Juni 06,2026 katika kikao kilichofanyika Zanzibar kuhusu uendelezaji na utangazaji wa zao jipya la Utalii wa Halal, kilichoandaliwa na Taasisi ya Samia Foundation, kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

Ameeleza kuwa Utalii wa Halal ni moja ya mazao mapya ya utalii yatakayochochea ongezeko la watalii nchini, hususani kwa kuvutia wageni wengi zaidi kuitembelea Tanzania na kupanua masoko ya kimataifa. Amesema aina hii ya utalii huvutia wageni wanaohitaji huduma zinazozingatia misingi ya imani, maadili na tamaduni zao wakati wa kutalii ikiwemo fursa za kufanya ibada katika maeneo ya huduma za utalii na malazi,  mapishi na vyakula kwa misingi ya halal, kuepuka matumizi ya vilevi, kuzingatia faragha za jinsia na familia, na fursa za kuandaa vifurushi vya safari kutembelea maeneo ya vivutio.

Ameongeza kuwa Zanzibar tayari imeridhia na kuchukua hatua za kimkakati za kuendeleza utalii wa halal ambapo pia wadau wa Sekta Binafsi  katika mnyororo wa huduma za utalii wameonesha mwitikio mkubwa, sauala ambalo lina fursa muhimu katika kuiwezesha nchi  kufikia malengo ya kuongeza idadi ya watalii na Pato la Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrick Soraga, amesema kupitia Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wataweka taratibu zote muhimu kuhakikisha Utalii wa Halal unatekelezwa na kutangazwa kwa ufanisi wa hali ya juu.

Akiwasilisha mada kuhusu Utalii wa Halal, Sheikh Ismail Bullock kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dar Al Ber Society yenye Makao Makuu yake jijini Dubai, amebainisha kuwa utalii huo umefanikiwa katika nchi mbalimbali duniani na kwamba kwa Tanzania pia utachangia kuongeza idadi ya watalii, Pato la Taifa na fursa za ajira.

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi, Richie Wandwi, amesema ni wakati muafaka kwa Tanzania kuendeleza zao la Utalii wa Halal hatua ambayo inakwenda sambamba na utekelezaji wa matakwa ya Sera ya Taifa yappp







Utalii ya mwaka 1999 inayotilia mkazo suala la kuongeza wigo wa mazao ya utalii nchini na utoaji wa huduma bora kwa wageni kwa kukidhi mahitaji ya soko la utalii wa Kimataifa.


No comments: