Zanzibar Soap ambao ni wauzaji wa bidhaa za Sabuni za urembo zilizotengenezwa kwa kutumia miti ya asili wemesogeza huduma kwa Wananchi katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea barabara ya Kilwa Temeke Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Meneja mauzo wa Zanzibar Soap, Bw. Mjaka Sogora amesema bidhaa hizo zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu huku zikiwa katika aina tofauti kama sabuni za kipande, sabuni za maji, na sabuni za miche.
"Wateja na wadau mbalimbali tunawakaribisha kwenye hema la Serengeti ambalo lipo jirani na hema la NIDA.
Ukifika utaona bango la Zanzibar Soap, lakini pia utaona bidhaa zetu mbalimbali.
Njoo na pesa kidogo, ujaze kapu, kuna offa ya pungozo kubwa na bidhaa zetu wanatumia watu wote, Wanawake kwa Wanaume na watoto pia.
Lakini pia Zanzibar Soap tuna bidhaa tofauti tofauti zenye kutibu, kuponya na kurekebisha yule mwenye;-Chunusi, muwasho mwilini, ngozi iliyofifia na huondoa mabaka baka mwilini, Ewe Mteja Pendezesha mwili wako na ngozi yako kwa kutumia Zanzibar Soap." Amesema Mjaka Sogora.
Baadhi ya sabuni zinazopatikana kwenye banda lao hilo ni pamoja na: Turmeric/Honey Soap, Lemon/Honey Soap, Nuru Soap -Coffee Scrub, Molato, Kojic na Luxury Shea Butter.
Kwa wateja na mawakala,kwa wanaotaka bidhaa hizo za Zanzibar Soap wanaweza wasiliana na Zanzibar Soap waliopo Mtaa wa Tomondo Temeke Pire Dar es salaam, mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la Zanzibarsoap.








No comments:
Post a Comment