ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 2, 2026

SIGMAGAS & ENGINEERING WASOGEZA HUDUMA SABASABA, WATOA ELIMU JUU YA MABOMBA YA GESI



SIGMA Gas and Engineering inayojihususha na mifumo ya mabomba ya gesi ya hospitali (MGPS) gesi Tiba wapo kwenye maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea barabara ya Kilwa Temeke Jijini Dar es salaam kwa kutoa elimu mbalimbali juu ya matumizi ya gesi katika Sekta ya Afya.


Akizungumza Meneja Mauzo wa Sigma gas & Engineering, Bw.Frank Hyera amesema wamekuwa na utaratibu wa kushiriki maonesho hayo ya Sabasaba ikiwa ni kusogeza huduma kwa Umma kwa kutangaza shughuli wanazofanya.


"Karibu Sabasaba kwenye banda letu, Selous 49/50, tupo hapa kutoa elimu  jinsi mifumo ya mabomba ya gesi inavyofanya kazi na viwango vya usalama vinavyotumika katika tasnia.


Sigma gas and Engineering zaidi tumajishughulisha na masuala ya Vifaa Tiba hususani vya gesi ambapo tunafunga na tumefunga maeneo mbali mbali ikiwemo Hospitali za binafsi na za Serikali lakini pia maeneo maalum yanayohusiana na gesi upande wa matibabu." Amesema Frank Hyera.



Aidha, pia wanafanya 

mifumo ya kuweka mabomba ya gesi ya viwandani, mifumo ya gesi ya maabara, na mifumo ya mabomba ya LPG.


"Sisi pia ni wasambazaji rasmi wa Renner Compressors, Peak Scientific, na British Oxygen Company (BOC) kwa hapa Nchini.

Mifumo ya Mabomba ya Gesi ya Hospitali,

Tunatoa suluhisho za kina kwa ajili ya usanifu, usakinishaji, na matengenezo ya mifumo hiyo, kwa kutumia mifumo ya kisasa tunaweka ilikurahisisha huduma hii ya gesi katika Sekta ya Afya.


Lakini pia tunafunga mifumo ya gesi viwandani, Mifumo ya Mabomba ya Gesi za Maabara, Mifumo ya Mabomba ya LPG hii ni kwa hoteli, shule, na majengo ya makazi.


"Lakini pia tunapatikana Buguruni Malapa, Dar es salaam unaweza kuwasiliana nasi

+255 677 071 127 au

info@sigmagas.co.tz 

Facebook: SigmaGas & Engineering 

Instagram: sigmagas_and_engineering" amemalizia Frank Hyera.


Mwisho.

No comments: