Wednesday, February 10, 2010

Goodluck Jonathan kuiongoza Nigeria


Makamu wa rais nchini Nigeria, Goodluck Jonathan, amekabidhiwa mamlaka kama kaimu rais, kuchukua nafasi ya Rais Umaru Yar'Adua ambaye anaugua .
Yar'Adua amekuwa akipata matibabu nchini Saudi Arabia tangu mwezi Novemba mwaka jana.

Awali Bunge la nchi hiyo lilipiga kura kumkabidhi mamlaka makamu huyo wa rais, ili kumaliza mzozo wa kikatiba uliokuwa ukiikumba nchi hiyo.

Akihutubia taifa kupitia runinga ya nchi hiyo, Bw. Jonathan ameahidi uongozi bora na kuimarisha vita dhidi ya Ufisadi.

Bw. Jonathan pia ameahidi kushughulikia mzozo wa muda mrefu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

No comments: