Thursday, February 11, 2010

Misri yamzuia kocha wake kuajiriwa Nigeria

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Misri limekataa kumruhusu kocha wake Hassan Shehata kusajiliwa kuwa kocha wa timu ya taifa Nigeria itakayoshiriki katika mechi za kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Shehata alikuwa miongoni mwa makocha saba ambao walikuwa wamependekezwa na shirikisho la soka la Nigeria, kuongoza timu ya taifa ya nchi hiyo katika kombe la Dunia. Awali shehata alikuwa amesema atakubali kandarasi na timu hiyo kwa muda mfupi.
Shehata amesema alikuwa ameulizwa na shirikisho la soka la Nigeria kuchukua wadhifa huo, lakini muajiri wake wa sasa amekataa. Mkataba wa Shehata na shirikisho la soka la Misri utakamilika mwaka wa 2012.
Kocha wa Bayern Munich, Louis Van Gaal, ambaye ni raia wa uholanzi, vile vile amekataa kuchukua wadhifa huo ulioachwa wazi baada ya Shaibu Amodu kufutwa kazi wiki iliyopita.
Kocha wa Urussi Guss Hiddink anatarajiwa kuteuliwa kama kocha wa Nigeria. Makocha ambao wamependekezwa kazi hiyo ni Guss Hiddink wa Urusi na makocha wengine wanne.

No comments: