Thursday, February 11, 2010

NAFASI NYINGINE ZA KAZI WIZARA YA MAMBO YA NJE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA KIMATAIFA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
anapenda kuwatangazia Watanzania wenye sifa kutoka Bara na Visiwani,
kuomba kazi zilizotangazwa hapa chini. Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa inazingatia usawa wa kijinsia katika kutoa
ajira. Hivyo Wanawake wenye sifa wanahimizwa kuomba.Nafasi
zinazotangazwa ni kama ifuatavyo
:-

1. AFISA MAMBO YA NJE MKUU DARAJA LA I,TGS H(NAFASI 2)

KAZI ZA KUFANYA:

i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje kwa kutilia maanani
masuala yaliyopewa kipaumbele katika kukuza na kuimarisha uchumi wa
Taifa.ii) Kufanya tathmini za utekelezaji wa Sera mbalimbali za
kiuchumi na kutoa ushauri na mapendekezo ya utekelezaji wake.iii)
Kuratibu Wizara na Taasisi mbalimbali kutekeleza majukumu/makubaliano
yaliyokubalika Kikanda na Kitaifa (Regional and International
Cooperation) kwa wakati uliokubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI:

i. Awe na shahada ya Uzamili (Masters) kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapoya fani zifuatazo:a.
Uhusiano wa Kimataifa;b. Public Policy;c. Uchumi;d. Biashara ya
Kimataifa; nae. Sheria ya Kimataifa.ii. Awe na ujuzi wa kutumia
kompyuta pamoja na uzoefuwa kazi kwa muda usiopungua miaka kumi na
mbili

(12).SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni
kamavile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na
Kiarabu.

2. AFISA MAMBO YA NJE MWANDAMIZO, TGS F(NAFASI 1)

KAZI ZA KUFANYA:1. Kuhudhuria mikutano ya Kimataifa.2. Kutafiti na
kuchambua taarifa mbalimbali.3. Kuratibu njia za wageni toka nje
zinazopitia Anga zaNchi yetu au kutua nchini.4. Kuratibu mabaraza ya
pamoja ya ushirikiano baina yanchi yetu na Mataifa ya nje.5. Usaili
katika ngazi za Kiwaziri na Kibalozi.SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe na
shahada ya Uzamili (Masters) kutoka VyuoVikuu vinavyotambuliwa na
Serikali katika mojawapoya fani zifuatazo:a. Uhusiano wa Kimataifa;b.
Public Policy;c. Uchumi;d. Biashara ya Kimataifa; nae. Sheria ya
Kimataifa.ii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu wa
kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7).

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile
Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.

3. AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II, TGS D(NAFASI 8)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu
masuala ya mahusiano ya Kimataifa.ii. Kuhudhuria mikutano
mbalimbali.iii. Kuandaa mahojiano.iv. Kufuatilia masuala mbalimbali ya
kimataifa.v. Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbaliyanayohusu
uchumi, siasa na jamii.vi, Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.

SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe na shahada ya Sanaa (B.A.) kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serkali, na
ambaye amejiimarisha (major) katika mojawapo ya fanizifuatazo:a.
Uhusiano wa Kimataifa;b. Uchumi; nac. Sheriaii. Awe amefanya na
kufaulu mtihani unaotolewa na Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.iii.
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.SIFA ZA ZIADA:i) Awe mwenye uwezo wa
kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi,
Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.ii) Mwenye
Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters/Postgraduate Diploma) kutoka
VyuoVikuu vinavyotambuliwa na Serikali katikamojawapo ya fani
zifuatazo:i. Uhusiano wa Kimataifa;ii. Public Policy;iii. Uchumi;iv.
Biashara ya Kimataifa; nav. Sheria ya Kimataifa

4. AFISA TAWALA MWANDAMIZI, TGS F (NAFASI 7)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuandaa bajeti ya matumizi ya Wizara.ii. Kuratibu
na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu katika Wizara.iii. Kufanya
kazi za uhusiano na itifaki Serikalini.iv. Kushughulikia masuala ya
nidhamu na ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Wizara.v. Kusimamia
utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kulingana na mahali alipo.vi.
Kuandaa taarifa za utendaji na matukio mbalimbali kila mwezi.vii.
Kutekeleza utaratibu wa uundwaji na utendaji wa Mabaraza ya
Wafanyakazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu.

SIFA ZA MWOMBAJI:
i. Awe mwenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters au Postgraduate
Diploma) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika
fanizifuatazo:-a. Utawala;b. Elimu ya Jamii;c. Sheria (baada ya
internship);d. Menejiment Umma; nae. Uchumiii. Awe na ujuzi wa kutumia
kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7).
Aidha, maafisa tawala wakaoajiriwa katika cheo hiki watatakiwa kufanya
au kufaulu mtihani wa maafisa tawala katika kipindi cha miaka miwili
tangu waajiriwe.

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile
Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.

4. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III, TGS B (NAFASI 2)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.ii.
Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu
wanapowezakushughulikiwa.iii. Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio,
miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi
zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na
kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.iv. Kusaidia kutafuta na
kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika
katika shughuli za kaziWizarani.v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya
Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa
zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.vi. Kusaidia kupokea
majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na
kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kuhudhuria
Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.ii. Awe
amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa
dakika moja na awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za
windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile
Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na
Kiarabu.MASHARTI YA WAOMBAJI WOTE:1. Maombi yaandikwe kwa mkono na
kuambatanishwa nakala za vyeti vya Shule, Vyuo, Vyuo Vikuu (Certificat
and transcript) na kozi ulizohudhuria.2. Wasifu binafsi wa mwombaji
(CV) pamoja na picha moja ya pasipoti ya siku za karibuni.3. Kwa wale
wote walioajiriwa maombi yao ya kazi ni lazima yapitishwe kwa waajiri
wao.4.

Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 45.5. Tarehe ya mwisho ya
kupokea maombi yote ni Februari 29, 2008.Maombi yote yatumwe kwa
anuani ifuatayo

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
S.L.P. 9000
DAR ES SALAAM.




1 comment:

Anonymous said...

Acha kutuzengua michongo wameshapeana wenyewe