Friday, February 12, 2010

Papic ajitosa rasmi kumrithi Maximo


KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic jana aliwasilisha rasmi barua ya maombi ya kazi Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwania nafasi ya kumrithi Mbrazil Marcio Maximo anayemaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars mwezi Julai.

Papic ambaye aliweka bayana dhamira yake hiyo ya kuwania kuifundisha Taifa Stars pale tu TFF ilipotangaza kuanza mchakato wa kumtafuta kocha mpya, aliwasili katika ofisi za shirikisho hilo majira ya saa 5:30 asubuhi akisindikizwa na katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako.

No comments: