Wednesday, February 10, 2010

Richmond yazikwa Dodoma

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imejivua suala la utata wa mkataba baina ya Tanesco na kampuni ya Richmond Development Company LLC, baada ya kueleza kuridhishwa na utekelezaji wa Serikali wa maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo huku ikielekeza kwamba masuala yaliyobaki, badala ya kubaki kama maazimio ya Bunge, yapelekwe kwenye kamati za kisekta zinazohusika.

Kamati hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), imeliomba Bunge azimio lililotaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na maofisa wa taasisi hiyo walioshiriki katika uchunguzi wa kuandaa taarifa ya Richmond wawajibishwe, kwa sasa liachwe kwenye mamlaka ya juu ya nchi.......chanzo Habari Leo

No comments: