Monday, February 8, 2010

Shekhe Yahya: Hakuna uchaguzi mwaka huu!


Mtabiri maarufu nchini,Shekhe Yahya Hussein,..ambaye mara nyingi amekuwa akitoa tabiri za utatanishi kiasi cha kuwatatanisha wananchi ameibuka tena na safari hii akikwambia hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu nchini.

Akichonga kupitia kituo kimoja cha televisheni katika kipindi cha masaula ya Nyota, juzi usiku, Shekhe Yahya alisema huo ni uatabiri wake mpya na aliusisitiza mara kwa mara.

Tangu mwishoni mwa mwaka jana Shehe Yahya amekuwa katikati ya mijadala ya kisiasa nchini, hasa ile inayohusiana na uchaguzi baada ya kutoa utabiri uliopingwa vikali, kuwa mwanachama yeyote ndani ya CCM atakayesimama kumpinga Rais Jakaya Kikwete kutafuta nafasi ya kugombea urais atafariki ghafla.

Huku akionekana kufafanua utabiri huo Shehe Yahya alisema, "nasema hakuna uchaguzi mwaka huu, uchaguzi utaahirishwa, siwezi kusema sana, maana karibuni nilitoa utabiri kuwa kuna mtu anaweza kufa katika kugombea urais, watu wamesema sana," alisema.

No comments: