Wednesday, February 10, 2010

Shindano la filamu fupi

katika mfululizo wa vipindi maalum vya televisheni na radio, vile vile online, wameanzisha shindano la kuandaa makala fupi ya video - iwe ni umeipiga kwa digital camera au mobile phone camera, ruksa!
Zawadi
Video au filamu tano bora zaidi kutoka kila bara - Afrika, Amerika ya Kusini + Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Asia na Oceania, zitaingia katika fainali ambayo itarushwa kupitia matangazo ya televisheni ya BBC World vile vile zitaonyeshwa kwenye tovuti ya BBC.

Mshindi wa jumla atapatikana baada ya hapo na kupewa zawadi ya semi-professional HD mini DV camcorder.

Masharti

Kila mshiriki anaweza kuwasilisha filamu/video moja katika lugha yoyote anayotaka kuhusu mada yoyote.
Wasilisha video uliyoifanyia kazi mwenyewe, usinakili wala kutumia kazi ya mtu mwingine.
Washiriki wanatakiwa kuandaa filamu/ video isiyozidi urefu wa dakika mbili (2), na wala isizidi 50MB katika format zifuatazo - avi, mov, wmv, mp4, mpg, flv, 3gp, wav, mp3, na wma.
Tarehe ya mwisho ya kupokea filamu/video ni March 10 (1600 GMT)

Jinsi ya kushiriki


Kwa maelezo zaidi, na jinsi ya kuwasilisha video yako tembelea wavuti ya BBC World News - My World

No comments: