Saturday, February 13, 2010

Wakristo wajitoa tamasha la mabomu

Imani Makongoro

UMOJA wa Wakristo Tanzania umepinga timu zao kushiriki tamasha la kuchangia walioathiriwa na mabomu Mbagala na wale wa mafuriko ya Kilosa lililokuwa limendaliwa na Baraza la Habari la Waislam nchini (Bakita).

Tamasha hilo lilipangwa kufanyika leo kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam na kushirikisha Waislam na Wakristo.

Mwenyekiti wa umoja huo, Samson Renatus, aliwambia waandishi wa habari jana kuwa sababu kubwa iliyofanya wao kushindwa kushiriki tamasha hilo ni kutokana na muda wa maandalizi ambapo wenzao Waislam walichelewa kuwapa taarifa mapema.

Alisema, wito wa kongamano hilo ulikuwa ni wa muda mfupi ukizingatia unahusisha umoja wa wakristo nchini kote.

1 comment:

Anonymous said...

Hayo mabaraza ya walaji tu wakristo na waislamu tuna njia nzuri za kuchangia maafa!