Advertisements

Friday, June 10, 2011

Tanzania Budget 2011-2012

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA 
MHESHIMIWA MUSTAFA HAIDI MKULO (MB.),
AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA 
SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO
 NA MATUMIZI KWA MWAKA 2011/2012

UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali   kujadili
na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2011/2012. Pamoja na hotuba hii, vipo vitabu vinne vinavyoeleza kwa kina takwimu
mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinahusu makisio ya mapato. Kitabu cha Pili
kinaeleza makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara na Idara zinazojitegemea
ambapo cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa na cha Nne kinaeleza makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa
Wizara. Idara zinazojitegemea, Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha,
upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2011 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.

   
 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa tena
kuongoza kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne. Aidha, ninampongeza Dkt.
Mohammed Gharib Billal kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Vile vile, nampongeza Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda
(Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na kuteuliwa tena na hatimaye kupitishwa na
Waheshimiwa Wabunge kuwa Waziri Mkuu kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu
ya Nne.
3.  Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi Mhe. Spika Anne Makinda
(Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Spika na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza
Bunge katika Afrika Mashariki. Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa
waliyonayo Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia busara zako, uwezo na uzoefu
wako ndani ya Bunge hili. Napenda pia kumpongeza Mhe. Job Ndugai (Mb.) kwa
kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. Nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja na
Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha,
napenda niwapongeze wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuingia katika
Bunge hili.
4.  Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati
kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho ya
Bajeti hii. Maandalizi ya Bajeti hii ya Serikali yanahusisha wadau na vyombo
mbalimbali. Kipekee ninaishukuru Kamati ya Fedha na Uchumi chini ya uenyekiti wa
Mhe. Dkt. Abdallah Omar Kigoda, Mbunge wa Handeni, pamoja na kamati nyingine za
kisekta kwa ushauri mzuri waliotoa wakati wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii.5. Mheshimiwa Spika, nao niishukuru kwa namna ya pekee Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kwa kutayarisha kwa wakati Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka
2011 na nyaraka mbalimbali za sheria ambazo ni sehemu ya Bajeti hii. Kwa upande wa
Wizara ya Fedha, nawashukuru Naibu Mawaziri Mhe. Gregory Teu (Mb) na Mhe.
Pereira Ame Silima (Mb). Namshukuru Katibu Mkuu Ndugu Ramadhani M Khijjah na
Naibu Katibu Makatibu Wakuu, Ndugu Laston T. Msongole, Dkt. Servacius B. Likwelile
na Ndugu  Elizabeth Nyambibo. Napenda kuwashukuru Prof. Benno Ndulu, Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania, Ndugu Harry Kitillya, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya ya Taifa. Aidha,
napenda kuwashukuru Wakuu wa Idara na wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha. Vile
vile, namshukuru Mpigachapa Mkuu wa Serikali kwa kuchapisha Hotuba hii kwa wakati.
Mwisho, nawashukuru wataalamu na wale wote waliotoa mapendekezo kuhusu Sera,
mikakati na masuala mbalimbali ya kodi ambayo yamezingatiwa katika kuandaa Bajeti
hii.
6.Mheshimiwa Spika, huu ni mkutano wa kwanza wa Bajeti kwa Bunge hili baada ya
uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2010 na
kukirejesha Chama cha Mapinduzi pamoja na Serikali yake katika kipindi cha pili cha
Awamu ya Nne. Wananchi wana matumaini makubwa kwa Bunge hili kwamba litasaidia
kuongeza kasi ya kuwapatia maendeleo na kuondokana na umasikini wa kipato
unaowakabili wananchi walio wengi. Hili linajidhihirisha kwa  uwepo wa Waheshimiwa
Wabunge wenye umri, jinsia, elimu na uzoefu mbalimbali. Ni matumaini ya Serikali
kuwa uwepo huo wa Waheshimiwa Wabunge utakuwa ni chachu katika kuwaltea
maendeleo wananchi kwa ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi.
7.Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka wa fedha unaoishia 2010/2011, imeendelea
kutumika kama chombo muhimu katika kutekeleza Sera na Malengo ya Uchumi na
Maendeleo ya Jamii. Katika kipindi hiki, yamekuwepo mafanikio ya kuridhisha katika
kutoa huduma bora kwa wananchi kuimarisha  miundombinu ili kuwezesha kukua kwa
uchumi na kupunguza umasikini.
8.Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 itazingatia vipaumbele vifuatavyo:
(i) Umeme;
(ii)Maji;
(iii) Miundombinu ya usafiri na usafirishaji (reli, bandari, barabara, viwanja vya ndege,
Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa);
(iv) Kilimo na umwagiliaji; na 
(v)Kupanua ajira kwa sekta binafsi na ya umma.
Bajeti itahakikisha pia kuwa mafanikio yaliyopatikana katika sekta za elimu na afya
yanalindwa pamoja na kuimarisha ubora wa huduma zinazotolewa.
Mikakati ya Kupunguza Makali ya Maisha kwa Mwananchi    
9. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wananchi katika
kupambana na makali ya maisha. Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, pamoja namambo mengine, inalenga katika kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo.
Kumekuwepo  na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji hatua za makusudi
kuchukuliwa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi na mwananchi mmoja
mmoja  ili kupunguza makali ya maisha kwa mwananchi. Hatua zitachukuliwa maeneo
yafuatayo:-:
(i)   Kasi kupanda kwa bei za bidhaa na huduma: Kasi ya ongezeko la bei za bidhaa
na huduma nchini pamoja na mambo mengine inasababishwa na: kuongezeka kwa bei
za mafuta  katika soko la dunia; kutopatikana kwa umeme wa uhakika na hivyo kuathiri
uzalishaji; na upungufu wa chakula nchini na nchi jirani. Serikali itachukua hatua
mbalimbali kukabiliana na hali hiyo kama ifuatavyo:
(a) Ongezeko la bei za mafuta ya petroli: Ongezeko la bei za mafuta ya petroli
linatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa bei katika soko la dunia.
Kwa mfano baada ya msukosuko wa uchumi duniani bei ya mafuta ilishuka hadi Dola
za Kimarekani 40 kwa pipa. Kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imefikia
takribani Dola 120 kwa pipa ambayo ni mara tatu ya bei  iliyokuwepo awali. Aidha,
ongezeko la bei linachangiwa  pia na kuongezeka kwa gharama za bima ya mizigo
nchini kutokana na tishio la maharamia baharini,  uagizaji wa mafuta wa kampuni moja
moja na migogoro ya kisiasa katika nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa bara la
Afrika. Pamoja na sababu zilizotajwa, bidhaa ya mafuta ya petroli inapoingia hapa
nchini hutozwa ushuru wa bidhaa (excise duty) na ushuru wa mafuta (fuel levy). Zipo
pia tozo mbalimbali zinazotozwa na Mamlaka zinazotoa huduma katika mfumo wa
uagizaji na upokeaji wa mafuta. Taasisi zinazotoza tozo hizo ni pamoja na EWURA,
SUMATRA, Shirika la Viwango la Taifa (TBS), kiwanda cha TIPER, Mamlaka Mapato
Tanzania, Mamlaka Bandari na makampuni yanayoagiza mafuta. Pamoja na hatua
zilizochukuliwa  na Serikali za kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na kuweka
viwango maalumu vya ushuru  wa bidhaa kwenye mafuta, bado bei ya rejareja ya
mafuta imeendelea kuwa kubwa na kuongezeka gharama za maisha. 
Mheshimiwa Spika, ili kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta nchini, Serikali
imeamua kufanya mapitio ya namna ya kukokotoa tozo zinazotozwa na Mamlaka
mbalimbali kwa lengo la kuzipunguza na zoezi hili litakamilika katika mwaka wa fedha
2011/12. Aidha, Serikali pia inakamilisha taratibu za ununuzi wa mafuta kwa wingi kwa
lengo kuyauzia makampuni ya usambazaji kwa beo ya jumla. Kanuni zitakazotoa
mwongozo  katika uagizaji mafuta kwa pamoja zimekamilika na utaratibu huu
unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2011/12. Utaratibu huu unatarajiwa
kupunguza bei na gharama za usafirishaji  wa mafuta  hayo. Pamoja na juhudi hizi za
Serikali, sekta binafsi inahimizwa kutumia gesi kama nishati mbadala wa mafuta ya
petroli hasa mijini. Ni matarajio yangu kwamba hatua hizi zitaleta unafuu wa bei ya
mafuta hapa nchini na hivyo kupunguza gharama za maisha kwa wananchi na
kuboresha uchumi kwa ujumla.  
(b) Upungufu wa Nishati ya Umeme:
Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokana na kiwango kidogo
cha uzalishaji usioendana na  mahitaji. Kwa kuzingatia kuwa umeme una umuhimu wakipekee katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali itachukua hatua kadhaa za kukabiliana
na upungufu huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100
Dares Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza; kuiwezesha TANESCO kupata mikopo
kutoka taasisi za fedha za kimataifa kwa ajili ya kununulia mitambo ya uzalishaji na
kuangalia upya namna ya kugawanya shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji na
Usambazaji; kwa lengo  la kuiachia TANESCO kujikita kwenye eneo ambalo ina uwezo
nalo kiushindani na hivyo  kuleta ufanisi katika sekta nzima ya umeme. Aidha, kutokana
na kukamilishwa  kwa sera, sheria na kanuni za ubia kati ya Serikali na sekta binafsi
((PPP), Serikali itaanda utaratibu wa kuhusisha sekta binafsi katika sekta ya umeme na
inatarajiwa kwamba baadhi ya miradi ya uzalishaji umeme itatekelezwa kwa njia ya ubia
kati ya Serikali na sekta binafsi. Serikali imeshaanza majadiliano na wawekezaji katika
uzalishaji  wa umeme kwa ubia katika miradi ifuatayo; Mtwara MW 300, Mpanga MW
144 na miradi ya usafirishaji umeme wa Kv 400 ya Morogoro-Tanga-Kilimanjaro-Arusha
km 682 na upanuzi wa Gridi ya Kaskazini  Magharibi kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na
Rukwa-km 1,000.   Serikali inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala vya
umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na biogesi pamoja na kutumia kwa
uangalifu nishati ya umeme iliyopo.
(c) Kuimarisha Hifadhi ya Chakula
Kutokana na kuendelea kuwepo kwa upungufu wa chakula kulikosababishwa na ukame
katika baadhi ya maeneo ya nchi, Serikali itaendelea kuimarisha hifadhi ya chakula kwa
kuongeza ununuzi wa mazao ya chakula katika Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya
Serikali (NFRA).Aidha, hifadhi hiyo itatumika kupunguza bei ya chakula nchini kwa
kusambaza nafaka kwa bei nafuu katika masoko wakati wa uhaba. Kadhalika, wananchi
wanashauriwa kuendelea kulima mazao yanayohimili ukame pamoja na kilimo cha
umwagiliaji na kuzingatia kuweka akiba ya chakula.
(ii) Kuongeza ajira: Ukosegu wa ajira, hasa kwa vijana umeendelea kuwa ni
changamoto kubwa, hivyo, Serikali inafanya juhudi za makusudi kupanua ajira katika
maeneo mbali mbali kama ifuatavyo:-
a) Mpango wa Ukanda wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (Southern Agricultural
Growth Corridor of Tanzania- SAGCOT). Mpango huu ni mkakati wa kuleta mapinduzi
ya kilimo ambao utatekelezwa  kwa ushirikiano kati ya serikali na wadau mbalimbali wa
kilimoi, wakiwemo washirika wa maendeleo. Utekelezaji wa mpango huu ambao ni
sehemu ya Kilimo Kwanza, utasaidia kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi
wanoishi vijijini kwa kuwaongezea mavuno ya mazao yao na kukuza ajira miongoni
mwa Watanzania.
Katika mwaka 2011/12 Benki ya dunia inatarajia kuchangia Dola za Kimarekani milioni
60 sawa na shilingi bilioni 92.8. Tunakamilisha taratibu za kupata fedha hizo na
tutawasilisha Bungeni kwa ajili ya kuidhinisha matumizi yake.
Mheshimiwa Spika, serikali pia itaendelea kufanya maboresho ya kilimo cha mazao,
ufugaji na uvuvi. Kwa upande wa mazao, Tanzania ina mabonde mazuri yenye rutuba
kwa kilimo cha mpunga katika mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Pwani,
Mbeya, Kilimanjaro, Tanga na Morogoro. Chini ya utaratibu huu, wakulima wadogowadogo watawezeshwa kupata huduma za mikopo, ugani, mbegu bora na mbolea.
Utafiti unaonesha kuwa kwa kutumia vizuri mabonde hayo, pembejeo na tija katika
uzalishaji, inawezekana kutoafursa za ajira mchanganyiko.
b) Viwanda vya kusindika mazao ya kilimo vitasaidia kuongheza thamani ya mazao na
ajira. aidha, eneo jingine la kuongeza ajira ni kupitia mwingiliano (linkage) baina ya
viwanda vya nguo na sekta ya kilimo. Juhudi zinazoendelea za kuimarisha upatikanaji
wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa maji na mafuta
ambavyo ni upepo, jua na biogesi, zitasaidia kufanikisha mpango wa uzalishaji wa
bidhaa viwandani. Kadhalika, Serikali itaboresha mazingira ya sekta ya viwanda
(vikubwa, vidogo na vya kati), ili kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
c) Kuingeza kasi ya utekelezaji wa MKURASBITA, ili mpango huu uweze kuchangia
ongezeko la ajira. Serikali kwa kushirikiana na AZAKI, AZISE na wadu wengine,
itaendelea kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs), ili kuiongeza ajira.
SIDO, VETA na vyuo vya maendeleo ya wananchi na vijana vitaboreshwa zaidi ili
visaidie kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambayo yataongeza ajira. Serikali imeweka
utaratibu mzuri wa kuwawezesha waombaji wa mikopo kwa kutumia dhamana ya
Serikali kupitia mifuko iliyo chini ya Benki Kuu na kupitia benki zao za biashara kupata
mikopo kwa ajili ya shughuli zao za uzalishaji. Utaratibu huu umenufaisha wajasiriamali
wengi ikiwa ni pamoja na vyama vya ushirika na sekta binafsi.
d) Kuharakisha maboresho yanayoendelea katika sekta ya fedha na utekelezaji wa sera
ya uwezeshaji ambazo zitasaidia upatikanaji wa mikopo kwa wananchiili waweze
kupata mitaji na kujiajiri. Hatua zinazochukuliwa na Serikali katika eneo hili ni pamoja na
kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa, kuanzishwa kwa taasisi ya kuratibu
taarifa sahihi za waombaji wa mikopo (credit reference bureau), ambayo itakuwa
inahifadhi taarifa sahihi za wakopaji (credit reference databank); na mwisho,
kuhamasisha mashirika ya umma, sekta binafsi na mifuko ya hifadhi ya jamii kuonheza
fursa za ajira katika maeneo yao kwa kuwekeza katika vitega uchumi na kutoa mafunzo
ya kujiajiri kwa vijana wasio na ajira.
10. Mheshimiwa Spika, ni matarajio yangu kwamba hatua hizi zitasaidia kuleta unafuu
na hivyo kupunguza gharama za maisha kwa wananchi na kuboresha uchumi kwa
ujumla. Serikali inaomba ushirikiano wa kila mmoja wetu ili hatua hizo zilete matokeo
yanayotarajiwa.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA SERA ZA BAJETI YA MWAKA 2010/11
11. Mheshimiwa Spia, mfumo wa Bajeti wa mwaka 2010/11 ulizingatia Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025; Makakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini
(MKUKUTA II); Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs); Ilani ya CCM ya Uchaguzi
Mkuu ya Mwaka 2005; Mkakati wa pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA); na
Mkakati wa Taifa wa Madeni.
12. Mheshimiwa spika, ktaika mwaka wa fedha 2010/11. serikali imeendeleakutekeleza majukumu yake kulingan na misingi ya sera ilizojiwekea. sera hizo zililenga
katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kusimamia matumizi ya fedha za umma na
uwajibikaji. aidha, serikali ilikusudia kuendelea kudhibiti Deni la Taifa pamoja na
kuboresha mahusiano yetu na wahisani wanaosaidia Bajeti ya serikali.
13. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi jumla pamoja na misingi na
sera za Bajeti, katika kipindi cha mwaka 2010/11. Serikali ilikadiria kukusanya mapato
na kutumia kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo jumla ya shilingi trilioni 11.6.
Kwa mwaka huo, serikali ilipanga kukusanya mapato ya ndani ya shilingi trilioni 6.0;
mapato kutoka Serikali za mitaa kiasi cha shilingi bilioni 172.6; misaada na mikopo ya
kibajeti shilingi bilioni 821.6; misaada na mikopo ya miradi ya maendeleo na ya kisekta
kiasi cha shilingi trilioni 2.5; mikopo ya ndani na nje shilingi trilioni 1.3; mikopo ya kulipia
dhamana na hatifungani shilingi797.6; na mapato kutokana na ubinafsishaji shilingi
bilioni 30.0.
14. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11, mafanikio
yaliyojitokeza ni pamoja na yafuatayo:
i) Kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani hadi mwezoi Machi 2011 kiliongezeka
kwa asilimia 21 ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa kipindi hicho mwaka 2009/10.
aidha, katika kipindi hicho, ukusanyaji wa mapato uliongezeka kutoka wastani wa
shilingi bilioni 390 kwa mwezi kwaka 2009/10 hadi shilingi bilioni 473 mwaka 2010/11;
ii) Kugharamia Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi oktoba 2010 kama ulivypangwa;
iii)Kufanikisha ununuzi wa tani 182,000 za chakula cha Hifadhi ya taifa, kwa kutumia
jumla ya shilingi bilioni 57, ili kukabiliana na tatizo la uhaba uhaba wa chakula
lililojitokeza katika baadhi ya maeneo nchini;
iv) Kugharimia mafunzo kwa wanafunzi 4,598 katika fani ya maafisa ugani wa kilimo na
mifugo;
v) serikali imeendelea kulipa madeni ya watumishi kulingana na uhakiki uliofanywa na
Mdhibiti an Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
vi) Mishahara na stahili za watumishi ziliendelea kulipwa kwa wakati.
vii) Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 200 kama sehemu ya gharama kwa ajili ya
ununuzi wa genereta zenyeb uwezo wa kufua umeme wa megawati 60 kwa mkoa wa
Mwanza na megawati 100 kwa mkoa wa Dar es Salaam. Aidha, serikali imechukua
hatua za dharura za kuounguza makali ya mgawo wa umemekatika gridi ya Taifa kwa
kugharamia ununuzi wa wa mafuta ya kuendesha mitambo ya kufua umeme ya IPTL,
ambapo jumla ya shilingi bilioni 18.5 zimetumika;
viii) Kwa ushirikiano na Serikali ya China, Serikali imeendelea na ujenzi wa jingo
maalum kwa ajili ya matibabu ya moyo katika hospitalin ya Muhimbili pamoja na wodi za
kulaza wagonjwa wa saratani katika hospitali ya Ocean Road;
ix) Kuongeza mtaji kwa shilingi bilioni 50 katika benki ya rasilimali (TIB) na hivyo kukuzamtaji hadi shilingi bilioni 92. Aidha, shilingi bilioni 20 ziliongezwa kwenye dirisha la
kilimo na kufanya dirisha hilo kuwa na shilingi bilioni 42; na
x) Kufanikisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi 96,328 ambapo jumla
ya shilingi bilioni 185 zimetumika, ikilingabnisha na wanafunzi 72,035 na shilingi bilioni
145 zilizotumika kwa kipindi kama hicho mwaka 2009/10.
MAPATO YA NDANI
15. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11, Serikali litarajia
kukusanya mapato y ndani ya kiasi cha shilingi bilioni 6,003.6 sawa na asilimoa 17.3 y
pato la taifa. Ili kuimarisha ukusanyaji wa mapatoya ndani, hatua mbalimbnali
zilizochukuliwa ni pamoja na:
i) Kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa kuhakikisha kuwa pale
inapowezekana malipo yanafanyika kupitia kwenye mabenki;
ii) Kuweka mkakati wa kuboresha huduma za utalii kwa kutathamini hoteli ili ziwe katika
viwango vinavyokubalika kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato yanayotokana na
ada;
iii) Kuhimiza utekelezaji wa Sheriaya fedha Na. 13 ya mwaka 2008 na Waraka wa
hazina Na. 8 wa mwaka 2008/09 inayoelekeza mashirika na taasisi kuchangia katika
mfuko mkuu wa serikali’
iv) Kuendelea kupanua wigo wa kodi kwa kusajili walipa kodi wapya na kuweka
mazingira bora ya biashara ili kuwezesha kukua kwa sekta binafsi;
v) Kuendelea kusimamia kwa karibumageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania, chini ya mpango wake wa tatu wa maboresho wa Miaka
Mitano ambayo yamekuwa msingi wa kukua kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani
mwaka hadi mwaka’
vi) Kuchukua hatua za kuboresha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kutoka Wizara
na Idara za Serikali’
vii) Kupitia upya utaratibu wa kutoa misamaha ya kodi kwa lengo la kuongeza udhibiti;
na
viii) Kuendelea kuhakikisha kwamba watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
wanajengewa uwezo kwa kuwapatia utaalamu wa kutosha ili kuonmgeza ufanisi katika
ukadiriaji na ukusanyaji wa mapato katika Serikali za Mitaa.
16. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11, Serikali ilifanya
marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la thamani, SURA 148. Marekebisho
mengi yaliyofanyika katika Sheria hii yalilenga kutoa kipaumbele katika kukuza
uzalishaji katika ekta ya kilimo na mifugo na kuongeza mchango wake kwenye Pato la
Taifa. Hivyo, marekebisho hayo yalijumuisha kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwa mashine na vifaa vya kukusanyia, kusafirishia na kusindika maziwa pamoja na
vifungashio vya maziwa ili kuhamasisha uwekezaji katika ekta ndogo ya maziwa na
hivyo kuboresha kipato cha wananchi.
17. Mheshiwa Spika, Serikali ilisamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
mashudu kwa ajili ya chakula cha mifugo ili kuhamasisha ufugaji bora na kuwawezesha
wakulima wa mbegu za mafuta kupata bei yenye tija kwa mauzo ya bidhaa hiyo;
kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye zana za kilimo, na huduma zakuzalisha mifugo ka njia ya kupandisha mifugo na kutumia mashine maalumu za
kuzalishia/kutotolea vifaranga pamoja an vifungashio vya juisi za matunda. Aidha,
serikali ilitya unafuu maalum wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mabanda
yanayotumika katika kilimo cha maua na kusamehe kodi za usafirishaji wa maua kwa
ndege kwenda nje ya nchi. Hatua hizizilipelekea kuongezeka kwa uzalishaji na
usindikaji wa maziwa, uagizajiw a matanki ya kuhifadhia maziwa, upatikanaji wa zana
za kilimo, pamoja na uzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo kwa baadhi ya maeneo
nchini.
18. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa unafuu maalum wa kodi ya ongezeko la thamani
kwenye uuzaji wa bidhaa na huduma zitolewazo kwa wakulima waliosajiliwa au
mashamba yavyama vya ushirika kwa ajili ya kujengamiundombinu ya mashamba kama
vile mifereji ya umwagiliaji, barabaraza mashambani, ujenzi wa mghala au huduma
nyingine za namna hiyo; na kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha
asilimia sifuri kwenye usindikaji wa mafuta ya kula kwa wazalishaji wa mafuta ya kula
wanaotumia mbegu zinazozalishwa hapa nchini. Hatua hizi wka pamoja zimesaidia
kupunguza gharama za uzalishaji na kubosha thamani ya bidhaa.
19. Mheshimiwa Spika, hatua hizi zimepelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa zana
za kilimo, pamoja na uzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo kwa baadhi ya maeneeo
nchini. Takwimu za awali zinaonyesha kuwa uzalishajiw a alizeti unatarajiwa
kuongezeka kutoka tani 328,533 mwaka 2009/10, hadi tani 666,030 mwaka 2010/11;
uzalishaji wa karanga kutoka 475,918 mwaka 2009/10, hadi kufikia tani 600,300 mwaka
2010/11; na ufuta kutoka tani 146,919 mwaka 2009/10, hadi kufikia tani 326,660 mwaka
2010/11. Hadi kufikia Aprili 2011, uagizaji wa vifaa vinavyotumika kuunganisha
mabanda maalum yanayotumikakuzalisha maua (green houses) uliongezeka kutoka
nyumba zenye uzito wa kilo 4,542,959 mwaka 2009/10, hadi kilo 7,181,228. Hata hivyo,
matokeo ya hatua nyingize zilizochukuliwa katika kuboresha uzalishaji kwenye kilimo
yatajitokeza katika muda wa kati na mrefu.
20. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11, Serikali pia ilifanya
marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kwa kuweka wigo wa ukomo wa
maeneo ya uchimbaji wa madini ka nia ya kudhibiti gharama zinazotakiwa kutolewa
katika kukokotoa faida inayotozwa kodi ya mapato kuwa ni zile zinazohusika;
kupunguza kiwango cha chini cha kodi ya mapato yanatoyotokana na ajira kutoka
asilimia 15  hadi asilimia 14, ili kuwaongezea kipato na kuwapunguzia mzigo wa kodi
watumishi wenye kipato cha chini; na kuwataka wafanyabishara wenye namba za
utambulisho wa mlipa kodi (TIN), kuzuia asilimia 2 kila wanapofanya malipo kwa
wasiokuwa na namba hizo, kutokana na bidhaa au huduma walizopata kutoka kwao, ili
Kuwahamasisha wasiokuwa na namba kwenda kusajiliwa.
21.Mheshimiwa Spika, Hatua hii, pamoja na juhudi nyinginezo ziliwezesha kuongeza
idadi ya walipa kodi wapya ambapo hadi machi 2011, jumla ya walipa kodi waliosajiliwana TIN wamefikia 686,098, ikilinganishwa na lengo la maboresho ya kodi ya mapato
kwa sekta ya madini yanatarajiwa kuongeza mapato katika muda wa kati na mrefu.
22.Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11, serikali ilifanya marekebisho
katika sheria ya ushuru wa bidhaa, SURA 147 kwa kupunguza ushuru wa bidhaa
kwenye mafuta mazito ya kuendeshea mitambo kutoka shilingi 97,hadi shilingi 80 kwa
lita moja,ili kupunguza gharama gharama za uzalishaji wa bidhaa nchini,katika
kuzingatia dhamira ya serikali ya kukuza viwanda na kuongeza ajira na mapato ya
ndani.Aidha katika kipindi hicho,serikali ilifanya marekebisho ya sheria ya magari
SURA124 pamoja na sheria ya usalama barabarani, SURA 168 kwa kupandisha ada ya
usajili,uhamisho na umiliki wa ada ya mwaka ya leseni za magari ili kuongeza mapato.
23.Mheshimiwa Spika,kwa kuzingatia matakwa ya itifaki ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki,mwaka 2010/11, Mawaziri wa Fedha wa Nchi wanachama waliridhia kufanya
marekebisho mbalimbali katika sheria ya forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
mwaka 2004 ili kuboresha sekta za viwanda, kilimo na usafirishaji kama vichocheo
muhimu katika kukuza uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
24.Mheshimiwa Spika,katika kipindi cha Julai 2010 hadi kufikia machi 2011 mapato ya
ndani yakijumuisha mapato ya serikali ya mitaa yalifikia shilingi bilioni 4,256.3,sawa na
asilimia 69 ya lengo la bajeti ya mwaka 2010/11 la shilingi bilioni 6,176.2.Kati ya fedha
hizo,shilingi bilioni 227.4 ni mapato yasiyo ya kodi na mapato ya serikali za mitaa
yalikuwa shilingi 118.2.
25.Mheshimiwa Spika,mapato halisi ya ushuru wa forodha yalikuwa shilingi bilioni
343.2, sawa na asilimia 70 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni
493.1.Mapato kutokana na ushuru wa bidhaa kutoka nje yalifikia shilingi bilioni
455.0,sawa na asilimia 73 ya bajeti ya shilingi bilioni 622.8,wakati shilingi bilioni 258.7
zilikusanywa kutokana na ushuru wa bidhaa zilizozalishwa nchini,ikilinganishwa na
bajeti ya shilingi bilioni 404.2,sawa na asilimia 64.Aidha mapato kutokana na kodi ya
ongezeko la thamani kutoka nje yalifikia shilingi bilioni 664.6,ikilinganishwa na bajeti ya
shilingi bilioni 999.3,sawa na asilimia 67,wakati shilingi bilioni 611.2 zilikusanywa
kutokana na kodi ya ongezeko la thamani kwa mauzo ya ndani, ikilinganishwa na bajeti
ya shilingi 992.3 sawa na asilimia 62.Mapato yalikuwa shilingi bilioni 1,255.8,ikiwa ni
asilimia 74 ya bajetiya shilingi bilioni1,702.7.Aidha mapato halisi yatokanayo na vyanzovingine vya kodi yalikuwa shilingi bilioni 449.7 ikiwa ni asilimia 72 ya bajeti ya shilingi
bilioni 620.9.
26.Mheshimiwa Spika,mapato yasiyo ya kodi kwa kipindi cha Julai 2010 hadi machi
2011, yalikuwa shilingi bilioni 227.4, ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 365.0
sawa na asilimia 62.Aidha, mapato ya serikali za mitaa yalikuwa shilingi bilioni 118.2
sawa na asilimia 68 ya bajeti ya shilingi bilioni 172.6.
MIKOPO YA NDANI
27.Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2010/11, serikali ilipanga kukopa shilingi bilioni
1,397.6 kutoka vyanzo vya ndani ili kugharamia bajeti yake.Kati ya kiasi hicho,shilingi
bilioni 600.0 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 797.6 ni
kwa ajili ya kulipia hatifungani zitakazoiva.Hadi machi 2011, kiasi cha shilingi bilioni
1,107.5 kilikopwa kwa ajili  hiyo.Kiasi hiki kinajumuisha dhamana za serikali zenye
thamani ya shilingi bilioni 607.6 zilizouzwa katika soko ili kulipia zilizoiva na shilingi
bilioni 499.9 zilitumika kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.
MISAADA NA MIKOPO YA MASHARTI NAFUU KUTOKA NJE
28.Mheshimiwa Spika,sheria ya mikopo,Dhamana na misaada ya mwaka 1974(kama
ilivyorekebishwa mwaka 2004) na kanuni zake, imeendelea kuwa msingi na nguzo kuu
ya ukopaji mikopo, utoaji dhamana na kupokea misaada ikiwa misamaha/unafuu wa
madeni.
29.Mheshimiwa Spika,katika kipindi cha Julai 2010 hadi kufikia machi 2011, misaada
na mikopo ya kibajeti ilikuwa shilingi bilioni 845.7,sawa na asilimia 103 ya
makadirio.Ongezeko hili limetokana na nchi ya Canada kuongeza mchango wake wa
misaada ya kibajeti mara mbili ya makadirio ya awali.Misaada na mikopo kwa ajili ya
miradi ya maendeleo, ikijumuisha mifuko ya kisekta ilifikia shilingi bilioni 1,427.6 sawa
na asilimia 58 ya makadirio.TATHMINI YA UWEZO WA NCHI KUKOPA NA KULIPA MADENI(SOVEREIGN
CREDIT RATING)
30.Mheshimiwa Spika,kufuatia kuanza kutengemaa kwa uchimi wa dunia baada
msukosuko wa kiuchumi duniani na nia ya serikali kuboresha upatikanaji wa taarifa
zilizohakikiwa kuhusu mwenendo  mzuri wa Taifa kiuchimi,kisiasa na utawala bora,
serikali inaendelea kumtafuta Mshauri Mwelekezi wa kimataifa kwa ajili ya kusimamia
zoezi la kutathmini uwezo wa nchi kukopa na kulipa madeni(Sovereign Credit
Rating).Mambo muhimu yanayozingatiwa katika tathmini hii ni pamoja na hali ya utulivu
na kisiasa;kasi ya kukua kwa uchumi;udhibiti wa usimamizi wa bajeti ya serikali;udhibiti
wa masoko ya fedha na hali ya mfumuko wa bei;na urari wa malipo ya nje ya
nchi.Hatua hii itasaidia kuwavutia wawekezaji na wakopeshaji kutokana na kuwepo kwa
taarifa ya hali ya kiuchumi,siasa na utawala wan chi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa
mikopo nafuu kutoka nje ya nchi kwa serikali na kwa sekta binafsi.
Deni la Taifa
31.Mheshimiwa Spika,mwaka 2000/01, Deni la Taifa lilikuwa Dola za Kimarekani
bilioni 8.55 ikilinganishwa na Dola bilioni 10.01 mwaka 2005/06 na kupungua mwaka
2006/07 hadi kufikia Dola bilini 7.53.Kupungua kwa deni hilo kulitokana na misamaha
mbalimbali ya madeni kutoka kwa nchi wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa
chini ya utaratibu wa(HIPC  na MDRI).Aidha, Deni la Taifa liliongezeka hadi kufikia Dola
bilioni 10.54 mwaka 2009/10, kutoka Dola bilioni 9.36 mwaka 2008/09.Kati ya deni la
mwaka 2009/10,Dola bilioni 5.99 ni deni la nje na Dola bilioni 4.55 ni deni la
ndani,ilijumuisha Dola bilioni 1.63 za dhamana za serikali kwa miradi ya Wizara, Idara
na Taasisi za Serikali.
UTEGEMEZI WA BAJETI
32.Mheshimiwa Spika,pamoja na mafanikio niliyoyaeleza kwenye mwenendo wa
mapato hapo juu,Bajeti ya serikali imekuwa ikitegemea misaada ya wahisani,ambayo
hivi sasa(2010/11)ni asilimia 17 ya bajeti kutoka asilimia 28 ya mwaka 2007/08.Kwa
kuzingatia umuhimu wa taifa kujitegemea kifikra na kirasilimali katika kuleta maendeleo,
Serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kuongeza mapato ya ndani, ikiwa ni
pamoja na kupanua wigo, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na kutambua walipa kodi
wapya ;na kudhibiti matumizi ili ifikapo mwaka 2015.Kiwango cha utegemezi wa misaada ya wahisani kwenye Bajeti ya serikali kisizidi
asilimia 10.
MATUMIZI
33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011, sera za matumizi ya
Serikali zililenga katika kuboresha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za uuma
ili kuongeza ufanisi pamoja na kutoa kipaumbele kwa maeneo muhimu ya kuichumi
yanayochochea  kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umakini, hususan wa kipato.
Katika kipindi cha Juni 2010 hadi Machi 2011, jumla ya matumizi ilikuwa shilingi bilioni
7,169.3, sawa na asilimia 67 ya makadirio ya mwaka. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni
5,226.9 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 1,942.4 ni matumizi ya maendeleo.
34. Mheshimiwa Spika, hadi Machi 2010, malipo ya mishahara ya watumishi wa
Serikali yalikuwa shilingi bilioni 1,749.1, sawa na asilimia 79 ya Makadirio ya mwaka.
Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 569.96 zilizotolewa kwa ajili ya Wizara na Idara
zinazojitegemea, shilingi bilioni 52.9 kwa ajili ya Sekretarieti za Mikoa na shilingi bilioni
1,126.2 kwa ajili ya Halmashauri. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 443.9 zililipwa kwa ajili
ya mishahara ya taasisi na mashirika ya umma.
35. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai, 2010 hadi Machi 2011 malipo ya riba
kwa madeni ya ndani yalifikia shilingi bilioni 173.6, sawa na asilimia 74 ya makadirio ya
mwaka. Aidha, kiasi cha shilingi bilioni 44.6 kilitumika kulipia riba kwa madeni ya nje,
swan a asilimia 34 ya makadirio ya mwaka. Kwa upande wa madeni mengine(CFS
Others), jumla ya shilingi bilioni 361.3 zilitumika ikiwa ni asilimia 66 ya makadirio ya
mwaka na kiasi cha shilingi bilioni 1,955.3 kilitumika kugharamia matumizi mengineyo.
Kwa ujumla, matumizi yalifanyika kulingana na upatikanaji wa mapato.
36.   Mheshimiwa Spika,  katika kipindi cha Julai 2010 hadi Machi 2011, matumizi kwa
ajili ya miradi ya maendeleo yalifikia jumla ya shilingi bilioni 1,942.4, ambapo shilingi
bilioni 514.8 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 1,427.6 ni fedha za nje, ikilinganishwa
na lengo la mwaka mzima la kutumia shilingi bilioni 1,366.1 na bilioni 2,452.9 kwa
mtiririko huo.37.  Mheshimiwa Spika,   kwa kutambua umuhimu wa vitambulisho vya Taifa, Serikali
imekamilisha taratibu za kumpata mzabuni na tayari mkataba umekwishasainiwa .
mradi huu  utagharimu jumla ya shilingi bilioni 355 mpaka utakapokamilika. Kwa mwaka
2011/12, jumla ya shilingi bilioni 70 zitatumika kama ilivyopangwa. Awamu ya kwanza
ya uzalishaji wa vitambulisho hivyo itakamilika mwishoni wa mwaka 2011. Mradi huu
ukikamilika utawezesha wananchi kuwa na utambulisho na hivyo kusaidia, pamoja na
mambo mengine kuongeza wigo wa ulipaji kodi, kurahisisha upatikanaji wa huduma
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha, na kuwatambua wahamiaji haramu.
MASUALA YANAYOHUSU SERIKALI ZA MITAA
38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Serikali kuu imeendelea kuzipa uwezo
Serikali  za mitaa wa kusimamia rasilimali watu na fedha ili ziweze kutoa huduma kwa
wananchi kwa ufanisi. Aidha,   Serikali imeendelea kuzipatia fedha, watumishi na
vitendea kazi na ushauri wa kitaalamu kulingana na maeneo yaliyoanishwa kwenye
bajeti.  Hadi kufikia Machi 2010, Serikali  za mitaa zilikuwa zimepokea  jumla ya shilingi
bilioni 1,358.6, sawa na asilimia 90 ya lengo la shilingi bilioni 1,504.7 zilizotarajiwa
kupelekwa kwa kipindi hicho.
39. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mapato ya ndani, Serikali za mitaa,
zimeendelea kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa mujibu wa sheria
ya fedha za Serikali za mitaa SURA 290. Katika mwaka wa fedha 2010/11, mapato
kutoka halmashauri yalikadiriwa kuwa shilingi bilioni 172.6. hadi kufikia mwezi Machi,
2011, mapato halisi yaliyokusanywa kwenye halmashauri yalifikia jumla ya shilingi
bilioni 118.2, ambayo, ni sawa na asilimia 68 ya bajeti. Aidha, Serikali imetekeleza
majukumu mengi ikiwa ni pamoja na:
i)    Kulipa kiasi cha shilingi bilioni 10.5 kwa ajili ya madeni ya watumishi wa
Serikali za Mitaa wasio walimu, kulingana na uhakiki uliofanywa na Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
ii) Ujenzi wa hospitali 3  za mikoa ya Manyara, Singida na Mbeya, pamoja na
ukarabati wa hospitali 10 za mikoa na 17 za wilaya;
iii) Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, nyumba 3 za wakuu wa mikoa, ofisi
22 za Halmashauri na nyumba 210 katika Halmashauri mbalimbali;
iv) Ukarabati wa ofisi 17 za wakuu wa mikoa, ofisi 26 pamoja na nyumba 23 za
wakuu wa Wilaya; nav) Kuboreshwa na kusambazwa kwa Mfumo wa IFMIS (Integrated Financial
Management Information System) kwenye ngazi ya Halmashauri ili
kuimarisha uwajibikaji, ufuatiliaji na tathmini ya  matumizi ya fedha za umma.
USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA
40. Mheshimiwa Spika, taarifa  ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu  wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2009/10, inaonyesha kutetereka kwa udhibiti na usimamizi wa fedha za
umma katika Wizara, Idara na Sekretarieti za Mikoa, ikilinganishwa na taarifa ya mwaka
2008/09. Taarifa inaonesha kupungua  kwa Hati safi za ukaguzi zilizotolewa kwa Wizara
na Idara za Serikali, kutoka asilimia 87 hadi asilimia 77, wakati hati zenye shaka
zimeongezeka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 20. Aidha, kwenye Mamlaka za Serikali
za Mitaa, hati safi za ukaguzi zimepungua kutoka asilimia 58 mwaka 2008/09, hadi 48.5
mwaka 2009/10, wakati hati zenye mashaka zimeongezeka kutoka asilimia 41 hadi
asilimia 48.5.
41.  Mheshimiwa Spika, baadhi ya sababu za kupungua kwa hati safi za ukaguzi ni
kutofuatwa kikamilifu kwa Viwango  vya Kimataifa vya utoaji wa taarifa za kihasibu
katika Sekta ya Umma (IPSAS), Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 na
kanuni zake za mwaka 2005, kukosekana kwa  usimamizi na ufuatiliaji wa karibu katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kutozingatiwa kwa mfumo wa udhibiti wa ndani,
ukosefu wa mafunzo endelevu kwa watumiaji wa mfumo wa IFMIS  kwenye Serikali za
Mitaa na kutotekelezwa kwa mapendekezo ya ukaguzi  kwa miaka iliyopita.
Usimamizi na Udhibiti wa Fedha za Umma- Serikali za Mitaa
42. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na udhibiti wa fedha za umma,
Sheria ya Fedha za Umma SURA 348 imepitiwa na kurekebishwa ili kuwapatia Mlipaji
Mkuu wa Serikali na Mhasibu Mkuu wa Serikali mamlaka ya kusimamia na kufuatilia
usimamizi wa fedha za umma katika ngazi ya Serikali za Mitaa. Kupitia marekebisho
haya, Serikali imeunda nafasi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi atakayeshughulikiausimamizi wa fedha katika Serikali za Mitaa, na hivyo kuwezesha utekelezaji wa dhima
ambayo imekusudiwa na mabadiliko haya.
Usimamizi wa Mashirika ya Umma
43. Mheshimiwa Spika, katika miaka ya hivi karibuni, zimejitokeza changamoto nyingi
katika kusimamia wakala, taasisi na mashirika ya 
Umma. Baadhi ya mashirika na taasisi za umma zinazotakiwa kujiendesha kibiashara
zimeshindwa kujiendesha kwa ufanisi na kuwa mzigo mkubwa na kutegena ruzuku
kutoka serikali kuu kinyume na lengo la kuanzisha mashirika na taasisi hizo.
44.Mheshimiwa Spika, Kutokana na changamoto hizo serikali imefanya mabadiliko
katika muundo wa wizara ya fedha kwa kuifanya ofisi ya msajili wa hazina kuwa wakala
anayejitegemea kwa lengo la kuzisimamia kwa karibu wakala, taasisi na mashirika ya
umma na hivyo kuongeza ufanisi, tija, mapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku
kutoka serikali kuu. Serikali inapitia sheria zilizoanzisha mashirika na taasisi mbalimbali
na sheria nyinginezo zinazohusiana na ofisi ya msajili hazina, ili kuondoa muingiliano
wa kiutendaji.
MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI (MKUKUTA 2)
45. Mheshimiwa Spika, Serikali ilikamilisha maandalizi ya Mkukuta awamu ya pili
(MKUKUTA II) na kuanza kutekelezwa mnamo Julai 2010. Kama nilivyojulish bunge
lako tukufu katika kikao cha bajeti mwaka 2010/2011 MKUKUTA II ni nyenzo kuu ya
kuliwezesha taifa kufikia dira ya Maendeleo ya taifa 2025 na ilani ya uchaguzi ya
Chama Cha Mapinduzi.
Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kugharimia MKUKUTA II hasa kwa
vipaumbele vinavyogusa wananchi walio wengi na kuboresha huduma za
jamii.Ugharimiaji wa mkakati huu unategemea bajeti ya serikali, michango ya jamii na
sekta binafsi.
46. Mheshimiwa Spika, Mkukuta II umejikita katika maeneo muhimu yafuatayo:
i. Miundombinu hususani, barabara za vijijini, reli, Bandar, viwanja vya ndege,
nishati ya umeme na miundombinu ya mawasiliano na habari pamoja na
usafirishaji wa nishati ya mafuta na gesi;
ii. Sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na Maendeleo ya mifugo na uvuvi
iii. Sekta ya viwanda, lengo likiwa kuendeleza viwanda vitavyotumia rasilimali za
ndani na;iv. Dhana ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa maana ya kupanua
na kuimarisha ushiriki na mchango wa wa sekta binafsi katika maeneo ya
miundombinu, uzalishaji wa mazao ya chakula, biashara pamoja na utoaji wa
huduma za jamii kama vile afya, usafirishaji, elimu na mafunzo na huduma za
kifedha 
Tume ya pamoja ya fedha
47. Mheshimiwa Spika,  Tume ya pamoja ya fedha ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, iliundwa kwa mujibu wa Ibara ya 134 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na sheria ya Tume ya Pamoja ya fedha sura 140. Tume imetoa taarifa kadhaa
na mapendekezo ikiwemo taarifa iliyotolewa mwaka 2006, kuhusu vigezo vya
kugawana mapato na kuchangia gharama za muungano.
Taarifa hiyo imefanyiwa mapitio mwaka 2010 ili kuiboresha na imewasilishwa kwa
wizara ya fedha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na wizara ya fedha, uchumi na
mipango ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwezi Aprili 2011. Kila
upande unaendelea kufanya uchambuzi wa mapendekezo ya tume na utawasilisha
maoni yake katika kikao cha pamoja, chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema mwaka 2011/2012.
UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
48. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2010/2011, Serikali iliendelea kutekeleza sera
ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu
kupitia mifuko na program mbalimbali; kuhamashisha uanzishwaji wa vyama vya
ushirika (SACCOS) na VICOBA kama njia bora ya kupata mikopo yenye masharti
nafuu, kuongeza kipato, ajira na kupunguza umasikini. Matokeo ya uhamasishaji huo ni
kuongezeka kwa vyama vya hivyo mara tatu kutoka 1875 mwaka 2005 hadi 5344
mwaka 2010, na kuongezeka kwa idadi ya wanachama na vyama hivyo kutoka
1,360,850 hadi 2,100,000.
Akiba na amana za wanachama zimeongezeka zaidi mara tano kutoka shilingi bilioni
31.4 mwaka 2005 hadi shilingi bilioni 174.6 mwaka 2010. Aidha serikali imekamilisha
mwongozo wa ufuatiliaji na tathmini ya mkakati wa utekelezaji wa sera ya taifa ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi. Vile vile maandalizi ya mwongozo wa kitaifa wa kutoa
mafunzo ya ujasiriamali yanaendelea.49. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2011/2012 Serikali itaendelea kutekeleza sera
ya taifa ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa kuieneza ili wananchi wengi
waielewe na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake; kutoa mafunzo kwa
wajasiriamali; kuhamasisha uwekaji akiba, uwekezaji na kuhamisha uanzishwaji wa
vyama vya ushirika; na kufanya tafiti zenye lengo la kuendeleza stadi a ujasiriamali na
kuanzisha na kuboresha shughuli za kiuchumi. Serikali itaendelea pia kuhamasisha
ushiriki wa wananchi katika shughuli za Maendeleo kupitia utaratibu unaosimamiwa na
mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF
MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA 2010/11 HADI JUNI 2011
50. Mheshimiwa Spika, kulingana na mwenendio wa makusanyo ya mapato kwa
kipindi cha miezi tisa ya mwaka 2010/11 inategemewa kuwa hadi Juni, 2011 serikali
itaweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5,553.7 sawa na asilimia 93 ya lengo la
shilingi bilioni 6,003.6.
51. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo na misaada ya kibajeti hadi kufikia
Juni 2011, kiasi cha shilingi bilioni 927.9 zinakadiriwa kupatikana ikilinganishwa na
shilingi bilioni 821.6 zilizokadiriwa hapo awali sawa na ongezeko la asilimia 13.
Mwelekeo unaonesha kwamba hadi kufikia Juni 2011 sehemu kubwa ya fedha
zilizokadiriwa kupatikana kutokana na misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya
Maendeleo zitapatikana.
52.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, Serikali imeendelea kutoa fedha
kulingana na upatikanaji wa mapato na kwa kuzingatia vipaumbele vilivyopangwa.
Mwelekeo ni kwamba matumizi yatakuwa chini ya lengo la bajeti ya mwaka 2010/11
kutokana na upungufu wa mapato. Aidha kabla ya mwisho wa mwaka 2010/11 Serikali
italipa madeni yaliyohakikiwa na vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na posho ya nyumba
kwa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma na pango la nyumba kwa waheshimiwa majaji.
MISINGI NA SHABAHA ZA BAJETI KWA MWAKA 2011/2012
53. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/2012 inazingatia maeneo muhimu ya
utekelezaji ili kufiia malengo ya dira ya taifa ya Maendeleo 2025, awamu ya pili ya
mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA II); Malengo ya
Maendeleo ya millennia 2015, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015; Mkakati
wa Pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA) na Mkakati wa Taifa wa Madeni.54. Mheshimiwa Spika, maeneo muhimu yatakayozingatiwa katika utekelezaji wa
bajeti ya mwaka 2011/2012 ni kama ifuatavy:
i. Kukabiliana na changamoto za kupunguza makali ya maisha kwa wananchi
kama nilivyoeleza hapo awali.
ii. Kuendelea kuboresha mfumo wa makusanyo na mapato ya ndani, kuboresha
mazingira ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje na uendelezaji wa sekta binafsi
ili kupanua wigo na kuongeza vyanzo vipya vya mapato
iii. Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya taifa; uanzishwaji wa
anwani za makazi na utekerezaji wa MKURABITA
iv. Kuhakikisha kwamba maduhuli ya serikali yanakusanywa ipasavyo na
kuwasilishwa katika mfuko mkuu wa serikali
v. Kutenga rasilimali katika maeneo ya kuongeza kasi ya ukuaji uchumi kama vile
miundombinu ya umeme, maji, barabara, bandari, kilimo, umwagiliaji, pamoja na
TEHAMA
vi. Kuimarisha utawala bora na uwajibikaji
vii. Kuendelea kutekeleza mipango na mikakati maalum  ya kuharakisha ukuaji wa
uchumi, kama vile kivutia wawekezaji kwenye miradi ya uzalishaji kwa ajili ya
kuuza nje (EPZ) na uanzishwaji wa maeneo maalum ya uwekezaji (SEZs)
viii. Kukamilisha uandaaji wa awamu ya nne ya programu ya maboresho ya
usimamizi wa fedha za umma (PFMRP IV) 
ix. Kuimarisha uandaaji wa na utekelezaji wa sera  za fedha ziendane na zile za
mapato na matumizi ili kupunguza mfumuko wa bei na ongezeko la riba pamoja
na kuongeza mikopo kwa sekta binafsi na kuhakikisha uhimilivu katika deni la
taifa.
x. Kuimarisha urari wa malipo kwa kusindika bidhaa kabla ya kusafirishwa nje, hasa
mazao ya kilimo, madini na bidhaa nyingine
xi. Kutafuta mikopo ya masharti nafuu na ya kibiashara kutoka benki mbalimbali ili
kuongeza uwezo wa Serikali kugharimia miradi mikubwa ya Maendeleo
xii. Kuharakisha utekelezaji wa sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na ya binafsi ili
kupanua fursa za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo 
xiii. Kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya sensa ya watu na makazi mwaka 2012; na xiv. Kulinda na kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii
(Elimu, Maji na Afya)
SERA ZA MAPATO
55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2011/12, Sera za mapato zinalenga
kukusanya mapato ya ndani, yasiyopungua shilingi bilioni 6,775.9, sawa na asilimia
17.2 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na matarajio ya kukusanya shilingi bilioni 5,553.7
au asilimia 16.0 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2010,11. Kati ya kiwango hicho, mapato ya
kodi ni shilingi bilioni 6,228.8, mapato yasiyo ya kodi ni shilingi bilioni 547.1 na mapato
kutokana na vyanzo vya Halmashauri ni shilingi bilioni 350.5.
56. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani
kwa kuchukua hatua mbalimbali za kiutawala kwa kuhusisha maeneo ya mapato ya
kodi na yasiyo ya kodi, pamoja na kupanua wigo wa mapato katika maeneo mengine.
Maeneo ya kisera yatakayozingatiwa ili kuongeza mapato ni pamoja na:-
i) Kuimarisha utaalamu na mbinu za kuhakiki kodi kodi kutoka kwenye kumbukumbu za
biashara(audit capacity); kuimarisha mfumo wa utawala wa kodi kwa kutumia
vitalu(Block Management System); kuingiza sekta isiyo rasmi kwenye mfumo wa kodi;
kutekeleza utawala wa kodi kwa kutumia mfumo wa viashiria hatarishi(Enterprise wide
Risk Management); na kudhibiti mbinu zote za ukwepaji Kodi;
ii) Kuhuisha Sheria mbalimbali zinazoruhusu misamaha ya kodi kwa nia ya kudhibiti
misamaha hiyo. Kwa sasa misamaha hiyo ni asilimia 2.5 ya Pato la Taifa na lengo ni
kufikia angalau asilimia 1 ya Pato la Taifa katika muda wa kati;
iii) Kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa
malipo yanafanyika kupitia benki; na kuanza kutumia mfumo wa kulipa kodi kwa
kutumia mfumo wa M-PESA kwa malipo ya Kodi yasiyozidi shilingi 500,000 ili kuondoa
kero ya walipakodi kukaa kwenye mistari.
iv) Kuimarisha TEHAMA katika utawala wa kodi- hasa katika utozaji kodi kwenye sekta
za Mawasiliano na Fedha, ukaguzi wa kina (Forensic Audit), na utunzaji na uchambuzi
wa takwimu;
v) Kuendelea kuimarisha matumizi na udhibiti wa Mashine za Elektoniki za  kutoa
stakabadhi za kodi(Electronic Fiscal Devices-EFDs) na kutoa elimu kwa walipakodi na
wafanya biashara  kuhusu matumizi ya mashine hizi;vi) Kusimamia Mpango wa tatu wa Miaka Mitano wa Maboresho ya utendaji wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika kukusanya
mapato;
vii) Kuboresha Mifumo ya Ukusanyaji na Usimamiaji kwa Mapato yasiyo  ya Kodi kwa
kupitia upya mfumo wa utoaji stakabadhi na leseni, pamoja na kuboresha viwango vya
kubakiza maduhuli(retention) kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali;
viii)Kupitia upya mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo(Properity tax) katika majiji,
manispaa, miji, wilaya na miji midogo na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wake, kwa
kutumia taarifa mpya za thamani za majengo hayo na kusimamia ulipaji wa kodi hiyo,
ikiwa ni pamoja na kupitia upya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyaji katika
Serikali za Mitaa;
ix) Kuendelea kuimarisha uchumi tulivu na kuweka mazingira bora ya biashara ili
kuwezesha sekta binafsi kukua na hatimaye kuweza kuchangia katika mapato;
x) Kuimarisha  miundombinu ya bandari, reli na barabara ili kuchochea biashara na
hatimaye kuongeza mapato; na
xi) Kuimarisha usimamizi na udhibiti wa bidhaa zipitazo katika bandari zetu kwenda nchi
za jirani, hasa bidhaa za mafuta, ili kuzuia uvujaji wa mapato ya serikali.
MISAADA NA MIKOPO
57. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2011/12, Serikali inatarajia kupokea
jumla ya misaada na mikopo yenye masharti nafuu kiasi cha shilingi bilioni 3,923.6,
ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 3,274.6 kwa mwaka 2010/11. Hili ni ongezeko
la shilingi bilioni 648.99, sawa na asilimia 20, ukilinganisha na kiwango cha mwaka
2010/11. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 869.4 ni misaada na mikopo ya kibajeti na
shilingi bilioni 3,054.1 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo
ikijumuisha mifuko ya kisekta.
58. Mheshimiwa Spika, napenda kuwatambua na kuwashukuru washirika wetu wa
maendeleo ambao wameendelea kutoa misaada na mikopo kwa ajili ya maendeleo ya
nchi yetu licha ya nchi zao kuathirika na msukosuko wa uchumi Duniani. Wahisani hao
ni: Uingereza, Denmark, Uholanzi, Ubelgiji, Canada, China, Finland, Ufaransa,
Ujerumani, Ireland, Italia, Japani, Korea Kusini, Norway, Sweden, Uswisi, Marekani,
India, Benki ya Dunia, Banki ya Maendeleo Afrika, BADEA, Umoja wa Ulaya, Global
Fund, Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), Kuwait Fund, Nordic Fund, Opec Fund, SautiFund, na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Wote  tunawashukuru sana kwa michango
yao.
MIKOPO YA KIBIASHARA
59. Mheshimiwa Spika, kiwango cha mikopo yenye masharti ya kibiashara kinazingatia
tathimini ya uhimilivu wa deni la Taifa, ambapo kiasi cha Dola za Kimarekani milioni
1,500 zinazokadiriwa kukopwa kwa muda wa miaka mitatu, 2010/11- 2012/13. Hivyo,
Dola za Kimarekani milioni 882, sawa na shilingi bilioni 1,271.6. zinatarajiwa kutumika
mwaka 2011/12. kati ya kiasi hiki, Dola milioni 297 sawa na shilingi bilioni 459 ni albaki
ya mikopo iliyotarajiwa mwaka 2010/11 na Dola milioni 525, sawa na shilingi bilioni 812
zinatarajiwa kupatikana mwaka 2011/12. Fedha hizi zitatumika kwa miradi ya
maendeleo ikijumuisha miradi ya miundombinu.
MIKOPO YA NDANI
60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/12, Serikali inakusudia kukopa kiasi cha
shilingi bilioni 1,204.3 katika soko la fedha la ndani. Kati ya kiasi hiki, shilingi bilioni
393.4 kwa ajili ya kuziba nakisi ya mapato ya Serikali na kiasi cha shilingi bilioni 810.9
ni kwa ajili ya kulipia dhamana zinazoiva.
SERA ZA MATUMIZI
61. Mheshimiwa Spika, sera za matumizi ya Serikali zinalenga katika kuboresha
usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma, yakijumuisha udhibiti wa ulipaji
wa mishahara, matumizi katika miradi ya maendeleo, ruzuku ya pembejeo, ununuzi wa
umma na kuendelea kudhibiti ulimbikizaji wa madeni. Msisitizo utawekwa kwenye
kutekeleza maeneo yaliyoainishwa kwenye misingi na shabaha za Bajeti ya mwaka
2011/12 ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
62. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele niliyoyaainisha katika
aya ya 9, mchanganuo wa bajeti kwa baadhi ya sekta mwaka 2011/12 ni kama
ifuatavyo:i) Miundombinu ya barabara, reli, bandari na mkongo wa taifa zimetengewa
Shilingi bilioni 2,781.4 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 1,505.1 mwaka
2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 85.
ii) Nishati na madini imetengewa Shilingi bilioni 539.3 ikilinganishwa na Shilingi
bilioni 327.2 mwaka 2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 65. 
iii) Maji imetengewa Shilingi bilioni 621.6 ikilinganishwa na Shilingi bilioni  397.6
mwaka 2010/11 sawa  na ongezeko la asilimia 56.
iv) Kilimo na umwagiliaji kimetengewa Shilingi bilioni 926.2 ikilinganishwa na Shilingi
bilioni 903.8 mwaka 2010/11,sawa na ongezeko la asilimia 2.5.
v) Elimu imetengewa Shilingi bilioni 2,283.0 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 2,045.4
mwaka 2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 12.
 Vi)  Afya imetengewa Shilingi bilioni 1,209.1 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 1,205.5
mwaka 2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 0.3.
   Kudhibiti matumizi
63. Mheshimiwa Spika, Serikali itahakikisha kwamba taratibu za kifedha za ununuzi
wa umma zinafuatwa kikamilifu pamoja na kuondokana na matumizi yasiyokuwa ya
lazima:
  a) Katika mwaka wa fedha wa 2011/12, serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali
za udhibiti wa matumizi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi wa mishahara (Payroll
Audit) ambapo maafisa masuuli watafanya ukaguzi wa malipo ya mishahara ya asasi na
taasisi zao kila mwezi. Chini ya utaratibu huu wakuu wa idara watawajibika pia kufanya
ukaguzi wa mishahara ili kuhakikisha kuwa watumishi wanaolipwa mishahara ni wale
walio chini yao. Wakuu wa idara na maafisa wahasibu watawajibika kwa malipo ya
mishahara hewa. Aidha serikali itaendesha ukaguzi wa mara kwa mara kwa malipo ya
mishahara kupitia idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali na pia kupitia sehemu
ya ufuatiliaji wa matumizi ya serikali na utendaji kazi katika idara ya bajeti ya serikali . 
Katika mwaka 2011/12, sarikali imepanga kufanya sense ya watumishi wote wa serikali
na taasisi kwa kuandaa siku maalum ya malipo ya mishahara dirishani “National Pay
Day” . Aidha serikali itasimamia utekelezaji wa waraka namba 2 wa Hazina wa mwaka
2010 kuhusu uwajibikaji na udhibiti katika usimamizi wa malipo ya mishahara (Lawson,
version 9) ambao utaimarisha udhibiti wa malipo ya mshahara.b) Eneo jingine ambalo litazingatiwa ni ukaguzi wa miradi ya maendeleo. Kazi hii
itafanywa na kitengo cha ukaguzi wa kiufundi ( Technical Audit Unit) ambacho kitakuwa
chini ya idara mpya ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.
Ukaguzi huu utajikita katika kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha katika miradi husika
yanaendelea na thamani halisi ya fedha iliyotumika (Value for money).
c) Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali aliyoitoa mwezi Machi
2011 imeonesha kuwa kuna udhaifu mkubwa wa usimamizi wa fedha za umma katika
serikali za mitaa.
Katika jitihada za kukabiliana na hali hii, serikali itaendelea kupunguza idadi ya akaunti
za benki katika halmashauri hadi zifikie sita. Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai,2011 serikali
za mitaa zitakuwa na akaunti zifuatazo: Akaunti ya mapato, Akaunti ya amana, Akaunti
ya mishahara, Akaunti ya matumizi ya kawaida, Akaunti ya matumizi ya maendeleo na
akaunti ya mfuko wa barabara.
Hatua hii itasaidia kudhibiti matumizi ya fedha, kuongeza uwazi na uwajibikaji na
kuboresha utoaji wa taarifa za mapato na matumizi. Aidha serikali imeendelea
kuimarisha mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji katika serikali za mitaa ili kupata thamani
stahiki ya fedha za umma. Vilevile, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,pamoja na
mambo mengine, atakuwa na majukumu ya kusimamia masuala ya ukaguzi wa ndani
katika serikali za mitaa.
d) Kila mwaka serikali inatumia sehemu kubwa ya bajeti yake katika ununuzi wa bidhaa
na huduma mbalimbali. Hivyo katika mwaka wa fedha 2011/12, na taasisi zake kupata
bidhaa na huduma zenye ubora unaotakiwa kwa bei nzuri. Aidha serikali itaendelea na
juhudi zake za kudhibiti matumizi yake kwa kusitisha ununuzi wa magari aina zote
isipokuwa kwa sababu maalum na kwa kibali cha ofisi ya waziri Mkuu. Vile vile, serikali
itasitisha ununuzi wa samani za ofisi hususani zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi,
kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija, kupunguza matumizi ya
mafuta kwa magari ya serikali , kupunguza safari za ndani na nje ya nchi ikiwa ni
pamoja na ukubwa wa misafara, na pia kuendelea kupunguza uendeshaji wa semina na
warsha isipokuwa pale inapobidi na kwa kibali cha ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na
kupunguza gharama za maonesho na sherehe mbalimbali.
e) Tangu kutungwa kwa sheria ya ununuzi wa umma SURA 410 yamejitokeza
mapungufu mbalimbali katika utekelezaji wa sheria hii. Mapungufu hayo ni pamoja na
yale yaliyobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka
2009/10 ambapo baadhi ya idara za taasisi za umma zimeonesha udhaifu katika
utekelezaji wa sheria hii.Aidha ili kushughulikia mapungufu haya, serikali iliwasilisha muswada wa sheria wenye
mapendekezo ya marekebisho ya sheria za ununuzi wa umma 2010 katika mkutano wa
Bunge uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu. Muswada huu ulijadiliwa na kamati ya
Bunge ya Fedha na Uchumi pamoja na wadau mbalimbali, ambapo ilitolewa michango
ya kina yenye lengo la kuboresha muswada. Serikali kwa kuthamini michango hii, iliona
ni vyema kuchapisha upya muswada huu na baada ya kukamilika kwa zoezi hili, serikali
inatarajia kuuwasilisha Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.
f) Kuendelea kuimarisha mtandao wa kompyuta wa mfumo wa usimamizi wa fedha
(IFMIS) katika ngazi zote za serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi na kuzuia
malimbikizo ya madeni, kutoa mafunzo kwa wahasibu juu ya uandaaji wa hesabu katika
viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma (IPSAS) ili viweze
kuzingatiwa kikamilifu kutumia utaratibu wa kufanya malipo kwa kutumia TISS na
kuanza kutumia utaratibu huu wa malipo katika ofisi za Hazina ndogo na sekretarieti za
mikoa.
g) Serikali itaendelea kudhibiti utoaji wa dhamana za serikali wa wizara, idara na taasisi
za serikali. Aidha wizara na taasisi za serikali zinatakiwa kuomba fedha za miradi
mbalimbali kwa utaratibu wa kuomba dhamana. Hatua hii itasaidia kupunguza maombi
ya dhamana ili kuepuka ongezeko la deni la taifa lisilohimilika.
Ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi  
64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/11, Bunge lilipitisha sheria ya
ubia kati  ya sekta ya umma na sekta binafsi ya mwaka 2010 (Public Private
Partnership Act Na.19 of 2010). Kupitia sheria hii, sekta binafsi kwa kushirikiana na
sekta ya umma itaweza kujenga na kuendesha miradi muhimu na kutoa huduma za
kijamii na kiuchumi kama kilimo, miundombinu, viwanda, madini, elimu, afya, mazingira,
TEHAMA, biashara, michezo na burudani, hivyo kutoa nafasi kwa serikali kuelekeza
nguvu katika vipaumbele vingine. 
Aidha, sheria hii inakusudia kuwawezesha wananchi kupata huduma za uhakika
endelevu na kwa gharama nafuu, hivyo kuinua uchumi wa nchi yetu kwa kasi kubwa.
65. Mheshimiwa Spika, Sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi,
imeanzisha vitengo viwili. Kitengo kimoja kiko Kituo cha Uwekezaji Tanzania ambacho
kitahusika na kutangaza na kutoa vivutio kwa wawekezaji.Kitengo cha pili kiko wizara ya Fedha ambacho kitahusika na kuifanyia tathmini miradi
ya ubia na kuhakikisha kuwa miradi inayoanzishwa hapa nchini inajiendesha kibiashara,
na kwa misingi ya thamani ya fedha na haisababishi mzigo kwa serikali. Serikali
inakusudia Kuvipata vitengo hivi wataalam zaidi na wenye ujuzi wa fani y Ubia
kimataifa.
Majadiliano kati ya Wizara na Kamati za Kisekta
67. Mheshimiwa Spika, Katika mchakato wa kupitisha bajeti katika baadhi ya kamati
za Kisekta za Bunge, kulikuwa na maoni kwamba bajeti za baadhi ya Sekta hizo
zilizopangwa kwa mwaka 2011/2012, ni ndogo na kutoa ushauri kwamba ziongezwe.
Serikali imetafakari hayo yote na imeazimia kufanya marekebisho kwa baadhi ya
mafungu ya bajeti kwa kuzingatia upatikanaji wa mapato mapya. Marekebisho hayo
yatawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa.
Maslahi ya Watumishi 
 68. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha kuboresha maslahi ya
watumishi kulingana na uwezo wa mapato yake kwa lengo la kuwawezesha kumudu
gharama za maisha. Maeneno ambayo yatatiliwa mkazo ni pamoja na malipo ya
mishahara na likizo kwa wakati, kuhakikisha watumishi wanalipwa mafao yao mara
baada ya kustaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi. Sambamba na hayo,
Serikali itatoa mafunzo kwa maafisa wa Hazina ndogo na mahakama zote
zinazoshughulikia mirathi, na kuweka mikakati ya pamoja kuwaondolea kero
wasimamizi na warithi wa mali ya marehemu.
Usimamizi wa Mashirika ya Umma
69. Mheshimiwa spika, katika mwaka wa fedha wa 2011/2012, Ofisi ya Msajili wa
Hazina pamoja na mambo na mambo mengine, imelenga kufanya yafuatayo katika
usimamizi wa wakala, taasisi na mashirika ya umma:
i. Kuwezesha wakala, taasisi na mashirika ya umma kuingia     mikataba ya
utendaji na wizara mama;
ii. Kutekeleza ukaguzi wa kimenejimenti kwa wakala, taasisi na mashirika ya
umma;iii. kuuandaa mfumo wa uperembaji nauhakiki wa menejimenti na Bodi za wakala,
taasisi na mashirika ya umma;
iv. Kuongeza makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kwa kuzingatia Sheria ya Fedha
Na. 13 ya mwaka 2008 pamoja na waraka wa Hazina Na. 8 wa 2008/2009;
v. Kuunda mfuko wa uwekezaji kwa ajili ya mitaji ya wakala, taasisi na mashirika ya
umma;
vi. Kutathmini mfumo wa uwiano wa mishahara ya wakala, taasisi na mashirika ya
umma;
vii. Kuratibu uperembaji na uhakiki wa mashirika yaliyobinafsishwa; na
viii. Kuendelea kushauri Serikali juu ya uwekezaji katika wakala, taasisi na mashirika
ya umma.
MASUALA YANAYOHUSU SERIKALI ZA MITAA
 70, Mheshimiwa spika, Serikali itaendelea kuboresha utendaji na uwajibikaji wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa
(LGRP II) ili kuwawezesha wakurugenzi kusimamia majukumu yao kikamilifu. Serikali
pia itawajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani ili wasimamie utendaji wa Halmashauri
zao na kuhakikisha nidhamu ya kazi inaimarishwa kulingana na sheria, taratibu na
kanuni za utumishi wa umma. Aidha, kamati za kupambana na rushwa pamoja na
kamati za maadili za Halmashauri zitaimarishwa ili kusimamia nidhamu ya watumishi
wa kada zote na kuhakikisha utendaji wao unazingatia maslahi ya taifa. Vile vile,
Serikali itaimarisha mapitio ya vigezo vya kupima utekelezaji wa majukumu ya
Halmashauri (Perfomance Assessment Criteria) ili kuongeza tija na ufanisi wa watendaji
wa Serikali za Mitaa.
  71, Mheshimiwa Spika, serikali za Mitaa zitaendelea kukusanya mapato kutoka
katika vyanzo vyake, ambapo jumla ya shilingi bilioni 350.5 zanakadiriwa kupatikana
kutoka vyanzo hivyo. Kiwango hicho cha mapato ni sawa na asilimia 5.2 ya mapato ya
ndani yanayokusanywa Serikali Kuu. Kiwango hicho kinaonyesha juhudi za serikali
zitakazochukuliwa ili kuboresha ukusanyaji ikilinganishwa na mwaka 2010/2011.Serikali
itaendeleza juhudi za ukusanyaji mapato katika ngazi ya Halmashauri, ili kuhakikisha
mapato hayo yanawiiana na fursa zilizopo. Baadhi ya hatua zitakazochukuliwa ni
pamoja na: kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato
kutoka vyanzo vya Halmashauri;  kupitia upya vyanzo vya kodi ya majengo katiaka
majiji, manispaa, miji, wilaya na miji midogo; na kuainisha mianya ya upotevu wa
mapato na vyanzo mbadala vya kuongeza mapato ya Serikali za Mitaa.72, Mheshimiwa spika, kwa upande wa matumizi, Serikali itaendelea kuboresha
utaratibu wa usimamizi wa matumizi ya Halmashauri. Baadhi ya hatua
zitakazotekelezwa ni pamoja na kuziwezesha na kuziimarisha idara za mipango,
uhasibu naukaguzi wa ndani ili kuongeza uwajibikaji, udhibiti na usimamizi wa fedha
katika Halmashauri; kuboresha na kupanua miundombinu ya barabara, maji na umeme;
kuendelea kutekeleza sera ya ugutuaji wa madaraka kwa wananchi kwa kujenga uwezo
wa Halmashauri katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yao; na kuendelea
kutekeleza program mbalimbali za maboresho.
MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA NYINGINE ZA
MAPATO:
73. Mheshimiwa spika,Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisera na
kiutawala ili kuongeza mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, na kupanua wigo wa mapato
katika maeneo mengine. Aidha, Serikali itaendelea kupitia sheria mbalimbali zinazotoa
misamaha ya kodi kwa lengo la kudhibiti misamaha hiyo;kusimamia mpango wa tatu wa
Miaka Mitano ya maboresho ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ;
Kuendelea kuingiza Sekta isiyo rasmi katika mfumo wa kodi; kupitia upya mfumo wa
ukusanyaji wa kodi ya majengo katika majiji, miji, manispaa, wilaya na miji midogo; na
kufanya mapitio ya vyanzo vya mapatomfumo wa ukusanyaji katika Serikali za Mitaa ili
kuongeza mapato.
  74. Mheshimiwa spika, marekebisho ya mfumo wa kodi yanahusu sheria zifuatazo:
a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SSURA 332;
c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
d) Sheria ys Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stai, SURA 82;
e) Sheria ya ushuru wa Stempu, SURA 189;
f) Sheria ya Ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220;
g) Sheria ya leseni za Biashara, SURA 208;
h) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168.
i) Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali za wizara, mikoa na idara
zinazojitegemea;
j) Sheria ya forodha ya jumuiya ya Afrika mashariki ya mwaka 2004;k) Sheria y kodi ya ongezeko la thamani, SURA 148
75. Mheshimiwa spika, ili kuhamasisha uwekezeaji na kuboresha uzalishaji katika sekta
za Kilimo, Mifugo, Viwanda Biashara na Utalii, na kuziwezesha kuchangia zaidi kwenye
pato la Taifa, napenedekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezko la
Thamani, SURA 148 kama ifuatavyo:-
i) Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vipuri vya zana za kilimo kama vile;
fyekeo (threshers), mashine za kukausha na kukoboa mpunga (rice dryers and mills),
mashine za kupandia mbegu (planters), na matrekta ya kukokota kwa mkono (power
tillers) vitakavyotumika kwenye kilimo cha mkataba, makundi yaliyosajiliwa na vyama
vya ushirika.
Hatua hii itahamasisha matumizi ya zana bora za kilimo na kuvutia uwekezaji kwenye
sekta ya kilimo;
ii) Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye chakula cha kuku (NASCOR Pellet
Feed). Hatua hii ina lengo la kuhamasisha uwekezaji katika ufugaji kuku hapa nchini;
iii) Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye nyuzi (Nylon Fishing Twine)
zinazotumika kutenengenezea nyavu za kuvulia samaki. Hatua hii inalenga kupunguza
gharama za uzalishaji na kuendeleza sekta ya uvuvi hapa nchini;
iv) Kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vipuri vya mashine za kunyunyizia
na kutifua udongo (sprayers and harrows) na mashine za kupanda nafaka (grain
conveyors); na
v) Kuanzisha utaratibu wa marejesho ya kodi kwenye mauzo rejareja kwa bidhaa za
ndani zinazouzwa kwa abiria ambao sio raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya nchi.
Utaratibu huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere na uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa mauzo ya thamani
ya shilingi 400,000 na zaidi.
76. Mheshimiwa spika, napendekeza pia kufanya marekebisho katika sheria ya kodi ya
ongezeko la thamani, SURA 148 kwa nia ya kuongeza mapato na kuhamasisha
mashirika na Taasisi mbalimbali ziweze kuchangia katika juhudi za serikali za
kuboresha huduma katika sekta ya elimu.
vi) Kuondoa msamaha wa kodi wa ongezeko la Thamani kwenye kuuza na Kupangisha
majengo ya kuishi ya nyumba za shirika la Nyumba la Taifa (NHC);
vii) Kuondoa unafuu wa kodi ya Ongezeko la Thamani uliokuwa unatolewa kwa
mashirika yasiyo ya kiserikali (Non-Governmental Organisations). Hatua hii haitazihusu
taasisi za kidini (Religious Organizations); naviii) Kutoa unafuu wa kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mashirika yasiyo ya kiserikali
Non Governmental Organisations) kwa vifaa vya matumizi ya kawaida (household
consumables) kama vile vyakula, mavazi na vifaa kama sabuni ambavyo vinatolewa
msaada kwenye vituo mahsusi vya kulelea watoto yatima na shule.
Hatua hizi katika Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa pamoja zitaongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 71,518.9
B. Sheria ya kodi ya mapato, SURA 332
77. Mheshimiwa spika, Napendekeza kufanya marekebisho ya sheria ya kodi ya
Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo:-
i)Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na
wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali..
ii) Kufuta kodi ya zuio kwa usafirishaji wa Samaki nje ya nchi kwa kutumia ndege za nje.
Hatua hii inalenga katika kuhamasisha mauzo nje ya Samaki nchi.
Hatua hizi za Kodi ya Mapato itapunguza mapatao ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 20,287.5
C. Sheria ya ushuru wa Bidhaa, Sura 147
78. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufany marekebisho katika sheria ya ushuru wa
bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo;-
i) kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya kuendeshea mitambo kutoka
Shilingi 80 hadi 40 kwa lita ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa hapa nchini;
ii) kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 50 badala ya 120 kwenye mifuko y plastiki za
microns 30 na zaidi yaani Polymers of ethylene na vinginevyo za (HS. CODE
3923.2900).
III) Kurekebisha kwa asilimia 10 viwango vya ushuru wa bidhaa mbalimbali isipokuwa
zile za mafuta ya petrol kama ifuatavyo;-
a) Vinywaji baridi kutoka shilingi63 kwa lita hadi shilingi 69 kwa lita;
b) Bia inayotengezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo haijaoteshwa, kutoka
shilingi 226 kwa lita hadi 249 kwa lita
c) Bia nyingine zote, kutoka shilingi 382 kwa lita hadi shilingi 420 kwa lita;d) Mvinyo ulitengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango
kinachozidi asilimia 25, kutoka shilingi 1,223 kwa lita hadi shilingi 1,345 kwa lita;
e) Mvinyo ulitengenezwa kwa zabibu inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango
kinachozidi asilimia 75 utatozwa shilingi 420 kwa lita na
f) Vinywaji vikali, kutoka shilingi 1,812 kwa lita hadi shilingi 1,993 kwa lita
iv)  kurekebisha viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye sigara kama ifuatavyo;-
a) Sigara zisizo na kifungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku
inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka shilingi
6,209 hadi shilingi 6,830 kwa sigara elefu moja
b) Sigara zenye kifungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa
hapa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kutoka shilingi 14,649 hadi
shilingi 16,114;
c) Sigara nyingine zenye sifa tofauti na (a) na (b) kutoka shilingi 26,604 hadi shilingi
29,264 kwa sigara elfu moja;
d) Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filter) kutoka shilingi 13,436
hadi shilingi 14,780 kwa kilo na
e) Ushuru wa (cigar) unabaki asilimia 30.
Hatua hizi katika ushuru wa bidhaa kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato
ya serikali kwa kiasi cha shilingi million 99,521.5
D. Sheria ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, sura 82
79. Mheshimiwa spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye sheria ya
elimu na mafunzo ya ufundi stadi, sura 82 kama ifuatavyo;
i) Kufanya marekebiso katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na tozo ya
kuendeleza ufundi stadi (skills developmeny levy) ya asilimia 6 ili asilimia
4 zipelekwe kwenye bodi ya mikopo ya wanafunzi wa eleimu ya juu, naasilimia 2 zipelekwe mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi
(vocational education and training authority- “VETA”). Lengo la hatua
hiikuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
 Hatua hii katika elimu na mafunzo ya ufundi stadi haijatarajiwi kupunguza wala
kuongeza mapato ya serikali.
E. Sheria ya ushuru wa stempu, sura 189
80, Mheshimiwa spika, napendekeza kufanya marekebisho ya ushuru wa stempu, sura
189 kama ifuatavyo;-
i) Kusamehe ushuru wa stempu wakati umilki wa mali (asset) unapohamishiwa
katika chombo maalum (kampuni) cha kutelekeza na kusimamia uzalishaji wa
kipato (special purpose vehicle “SPV”) kwa madhumuni ya kutoa dhamana
zinazotengemea hiyo mali ambayo umiliki wake umehamishwa. Hatua hii
inalenga kataka kuhamishwa miradi ya uwekezaji inayohitaji fedha nyingi,
mfano; miradi ya barabara, madaraja, nishati na maji. aidha ni njia mbadala
ya mabenki ya upatikanaji wa fedha za kugharamia miradi.
Hatua hii ya ushuru wa stempu haitapunguza mapato ya serikali bali inalenga
katika kuhamasisha utunzaji wa akiba na kuchochea uwekezaji
(Savings Mobilization and Investment)
F. Sheria ya ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220
81. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufnaya marekebisho katika Sheria ya
Ushuru wa Mafuta ya petroli, Sura 220 kama ifuatavyo:
i. Kusamehe Ushuru wa Mafuta ya Pteroli unaotozwa  kwenye mafuta yanayotumika
kwenye kuendesgha meli na vifaa vingine vinavyotumika katika utafiti wa mafuta na
gesi na mshamaha huu utatolewa kupiitia Tangazo la serikali. Aidha, Maombi ya
msamaha yatahakikiwa na kuptishwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC) kabla ya kuwasilishwa wizara ya fedha. Hatua hii inalenga katika kutoa unafuu
wa gharama kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi.
ii. Ili kutatua tatizo la ucheleweshaji la marejesho ya kodi (tax refunds) kwenye mafuta
ya yanayonunuliwa na kampuni za madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
itaanzisha utaratibu wa kuweka kiasi cha fedha kwenye Account maalum (escrow
account) ambacho kinawiana na kiwango cha mahitaji ya mafuta kwa mwezi. Aidha
Kampuni itaruhusiwa kununua mafuta kwenye matanki ya kampuni za waagizaji mafuta
bila ya kulipia kodi kwa kiwango cha fedha ilichoweka kwenye akaunti. Endapo mahitaji
ya mafuta kwa mwezi yuatkuwa makubwa zaidi ya kiwango ilichoweka kwenye akaunti,Kampuni hiyo itawajibuika kuongeza fedha za ziada zenye kukidhi mahitaji yake. Hatua
hii inaratajiwa kutatua la ulejeshwaji wa marejesho ya kodi iliyolipwa kwenye mafuta.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaandaa utaratibu wa utekelezaji utakaohusisha
kampuni za madini na kampuni za mafuta.
Hatua hizi kwa pamoja zitanguza mapato ya Serikali kwa shilingi million 2,007.6
G. Sheria ya Leseni ya Biashara, SURA 208
82. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika sheria ya leseni ya
Biashara, SURA 208 ili kutoza ada ya leseni ya biashara kwa kiwango na maeneo
yafuatayo:-
a)Mamlaka za Miji (Majiji, Manispaa na Miji) zitoze shilingi 50,000 kwa mwaka kwa kila
aina ya biashara inayostahili kupewa leseni ya biashara (isipokuwa ya vileo)
inayoendeshwa katika maeneo ya mamlaka hizo.
b) Halmashauri za Wilaya zitoze na kukusanya Ada ya leseni ya biashara ya shilingi
30,000 kwa mwaka kwa biashara zinazoendeshwa katika maeneo ya miji midogo na
vituo vya biashara.
c) Halmashauri za vijiji zitoze na kukusanya shilingi 10,000 kwa mwaka kwa kila
biashara inayoendeshwa katika maeneo yake.
Lengo la hatua hii ni kuimarisha usimamamizi wa kanuni za biashara hapa nchini na
kuwianisha ukuaji wa biashara na mapato yanayokusanywa. Pia itaongeza  mapato
kwa Serikali za mitaa na kuongeza uwezo katika kuhimili mahitaji yao. Aidha,
utekelezaji wa hatua hii unazingatia Sera ya serikali ya ugatuaji maradaka kwa
wananchi (Decentralization by Devolution “D by D”).
H. Sheria ya Fedha ya Seriakli za Mitaa, SURA 290
83. Mheshimiwa spika, Napendekeza marekebisho katika sheria ya fedha ya serikali
za mitaa SURA 290 ili kuziwezesha Serikali za mitaa kutoza ada ya leseni ya biashara
kwa kiwango na maeneo yaliyo ainishwa kwenye sheria ya leseni ya biashara.
I. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama
Barabarani, Sura 168 ikli kuongeza ukomo wa kiwango cha fainin inayotozwa kwa
kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka
shilingi 20, 000 hadi shilingi 300,000.
J. Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria za kodi85. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho mengine madogo madogo
yasiyo ya kisera katika Sheria mbalimbali za kodi ili ziwe sanjari na azma ya kurahisisha
utekelezaji wake.
K.Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali za Wizara, Mikoa na Idara
zinazojitegemea.
86. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya viwango vya ada na tozo
mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha
kulingana na hali halisi ya ukuaji wa uchumi.
L.Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki, ya mwaka 2004
 87. Mheshimiwa Spika, kikao cha maandalizi ya bajeti cha Mawaziri wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki(Pre-Budget Consultations of EAC Ministers for Finance)
kilichofanyika tarehe 7 Mei 2011 jijini Kampala, Uganda; kilipendekeza marekebisho  ya
viwango vya Ushuru wa pamoja wa Forodha(EAC Common External Tarriff “CET”) na
Sheria ya Forodha ya jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC Customs Management Act,
2004.  Marekebisho hayo yanalenga katika kukuza Sekta za Viwanda, Usafirishaji,
Mifugo, Biashara na Utalii.  Aidha yanalenga pia katika kuboresha afya ya jamii na
kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
 88. Mheshimiwa Spika,maeneo yanayopendekezwa kufanyiwa marekebisho kwenye
viwango vya Ushuru wa Pamoja wa Forodha(EAC Common External Tariff) ni
yafuatayo:-
i) Tanzania iruhusiwe kutoza ushuru wa forodha kwa asilimia 10 badala ya asilimia 35
kwenye ngano inayotambuliwa katika HS code 1001.90.20 na HS Code 1001.90.90 kwa
muda wa mwaka mmoja.  Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za uingizaji nchini
wa bidhaa hiyo na kuwezesha walaji kupata vyakula kwa bei nafuu.
ii)Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha(duty remission) kwenye malighafi ya
kutengeneza sabuni(Palm Stearin, RBD) inayotambuliwa katika HS Code 1511.90.40
kwa kipindi cha mwaka mmoja.  Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa kodi kwenye
viwanda vidogo na vya kati vya kutengeneza sabuni hapa nchini.iii)Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS Code 2710.19.59 ili kutoa
msamaha wa ushuru wa forodha(duty remission) kwenye malighafi za kutengeneza
manukato na sabuni(white oil).  Hatua hii inalenga katika kupunguza gharama za
uzalishaji viwandani.
iv)Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty remission) kwenye malighafi za
kutengeneza maganda ya viberiti(duplex boards) yanayotambuliwa katika HS Code
4810.92.00.  Hatua hii inalenga katika kupunguza ghrama za ushalizaji na kulinda
Viwanda vya Viberity kutokana na ushindani wa viberiti vinavyoagizwa nje.
v)Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye waya za
chuma ambazo zimenakisiwa na zink(Galvanized Plated/Coated Wire)hutozwa ushuru
wa forodha kwa asilimia 10.  Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa malighafi
inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iandane na kanuni/taratibu za kutoza ushuru
zinazozingatia viwango vya usindikaji.
vi)Kupunguza ushuru wa forodha kwenye mifuko ya plastiki ya kuhifadhia malighafi za
matunda(aseptic bags) kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 inayotambuliwa katika HS
Code 3923.29.00 kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kupunguza gharama za uzalishaji na
kuhamasisha usindikaji wa mazao ya matunda hapa nchini.
vii)Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha(duty remission) kwa kipindi cha mwaka
mmoja kwenye shaba ghafi(copper Cathodes) inayotambuliwa katika HS Code
7403.11.00.Hivi sasa bidhaa hii inatozwa ushuru wa asilimia 10 ambapo shaba
iliyotengenezwa kwa ukamilifu(copper alloys/refined copper) hutozwa ushuru wa
asilimia 0, ambapo ni kinyume na matakwa ya sheria ya ushuru wa fordha ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki ya nwaka 2004.  Lengo leo hatua hii ni kuwianisha ushuru wwa
malighafi inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iendane na kanuni/taratibu za kutoza
ushuru zinazozingatia viwango vya usindikaji.
viii)Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha(duty remission)kwa waunganishaji wa
majokofu(refrigerators and freezers)ili walipe ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala
ya asilimia 25 kwenye vifaa vya kuunganisha majokofu hayo(component parts and
inputs for assemblers of refrigerators and freezers).  Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa hizo na kuongeza ajira hasa kwa vijana.
ix) Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS Code 2309.90.00 ili kutoa
msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi za kutengeneza vyakula vyamifugo(premixes). Lengo ni kutoa unafuu katika bei za chakula cha mifugo na
kuhamasisha ufugaji.
x)  Kuendelea kutoza ushuru wa fordha wa asilimia 10 badala ya 25 kwenye mabasi
yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 25 yanayotambuliwa katika HS Code
8702.10.99 na HS Code 8702.90.99.
xi)Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwenye
magari ya mizigo yenye uwezo kati ya tani 20 yanayotambuliwa katika HS Code
8704.22.90 kwa muda wa mwaka mmoja.
xii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye magari ya mizigo yenye
uwezo zaidi ya tani 20 yanayotambuliwa katika HS Code 8704.23.90 kwa muda wa
mwaka mmoja.
xiii)Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwenye mabasi
yatakayoagizwa kwa ajili ya mradi wa mabasi wa jiji la Dar es Salaam yanayotambuliwa
katika HS Code 8702.10.99 na HS Code 8702.90.99 kwa muda wa mwaka mmoja.
xiv) Kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code 8703.90.10 ili kutoa
msamaha wa ushuru wa forodha kwenye pikipiki maalumu za kubeba
wagonjwa(motorcycle ambulances). Hatua hii inalenga kuimarsiha utoaji wa huduma ya
kusafirisha wagonjwa hasa katika maeneo ya vijijini.
xv)Kutenganisha virutubisho vya chakula vinavyotambulika katika HS Code 2106.90.90
ili kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwenye virutubisho
vya vyakula vya binadamu (food supplements) ili kuendana na sera ya serikali ya
kuboresha afya za wananchi.
xvi) kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code 9616.10.00 ili kutoza ushuru
wa forodha wa asilimia 10 badala ya kutengeneza vifaa vya kunyunyizia (scent s[rays
and other similar toilet sprays and mounts and heads).
xvii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye matrekta ya kukokota
mizigo yanayotambuliwa katika HS Code 8701.20.90 kwa muda wa mwaka mmoja.
Hatua hii inalenga ktk kuboresha usafirishaji mizigo na kuongeza ufanisi katika sekta ya
usafirishaji.xviii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye migahawa ya majeshi
ya ulinzi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
89. Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa fedha walikubaliana kufanya marekebisho kwenye
sheria ya forodha ya jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act,
2004) kama ifuatavyo:
i) Kufanya marekebisho ktk kifungu cha pili (2) cha jedwali la tano la sheria ya forodha
ya jumuiya ya Afrika mashariki ili kuliwezesha jeshi la polisi kunufaika na msamaha wa
ushuru wa forodha kama linavyonufaika jeshi la ulinzi. Hatua hii inalenga katika
kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
ii) Kufanya marekebisho katika jedwali la tano (5) la sheria ya forodha ya jamuiya ya
Afrika mashariki kwa nia ya kutekeleza yafuatayo:
a) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye mitego ya mbung’o (tsetse fly traps).
Hatua hii inalenga katika kuchochea ukuaji wa kilimo na kuboresha mazingira ya
kuvutia utalii hapa nchini.
b) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenya vifaa vya kudhibiti usalama (security
equipments:- hand held metal detectors, walk through metal detectors, CCTV cameras,
bomb detectors and undercarriage mirrors). Hatua hii inalenga ktk kuboresha usalama
wa raia na mali zao.
c) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenya magari yanayoendeshwa kwa
kutumia beteri (battery operated vehicles/Golf carts). Hatua hii itaimarisha huduma za
kitalii na huduma za afya kwani magari haya yanaweza kutumika kebeba wagonjwa
ndani ya hospitali na kubeba wageni na mizigo katika maeneo ya hoteli.
d) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye magari yanayotumika kubeba abiria
katika viwanja vya ndege (Apron buses) ili kuboresha huduma kwa wasafiri na kuweka
mazingira yenye kuvutia wageni na hasa watalii.
e) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi za kutengeneza vifaa
vinavyotumia mionzi ya jua (inputs for manufacture of solar panels) kwa lengo la
kuhamasisha uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini.f) Kupunguza kiwango cha ada ya ukaguzi (Destination Inspection Fee) kinachotozwa
kwenya bidhaa za biashara zinazotoka nje kutoka asilimia 1.2 ya thamani ya huduma
ya kuzifikisha hadi bandari (FOB) na kuwa asilimia 0.6. Hatua hii inalenga katika
kupunguza muda wa kuondoa mizigo bandarini na kupunguza gharama za uingizaji
bidhaa na hivyo kupunguza bei za bidhaa kutoka nje.
Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
million 4,669.7
M. Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi
90. Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa
tarehe 1 julai,2011, isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo.
MFUMO WA BAJETI KWA MWAKA 2011/12
91. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi pamoja na misingi na sera z
bajeti, SURA ya bajeti inaonesha kwamba jumla ya shilingi bilioni 13,525.9 zanahitajika
kutumika katika kipindi cha 2011/12. Jumla ya mapato yanayotarajiwa ni shilingi bilioni
13,525.9. Kati ya mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi na yasiyo
ya kodi ya jumla ya shilingi bilioni 6,775.9, sawa na asilimia 17.2 ya pato la Taifa. Aidha,
mapato kutoka vyanzo vya  
Halmashauri ni shilingi bilioni 350.5.kadhalika,serikali inategemea kukopa kiasi cha
shilingi bilioni 2,475.9 kutoka vyanzo vya ndani na nje.kati ya fedha hizo shilingi bilioni
810.9 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za serikali zinazoiva, shilingi bilioni
393.4 ni mikopo kutokana na mauzo ya hatifungani za serikali na shilingi bilioni 1,271.6
zitatokana na  mikopo yenye masharti ya kibiashara.
92.Mheshimiwa spika ,washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuendelea kuchangia
bajeti kupitia na mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 3,923.6 kati ya fedha  hizo, shilingi
bilioni 869.4 ni misaada  na mikopo ya kibajeti  na shilingi bilioni 3,054.1 ni misaada na
mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo,ikijumuisha mifuko ya kisekta.
93. Mheshimiwa Spika ,kwa  upande wa matumizi ,katika mwaka 2011/12 Serikali
imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na
maendeleo .kati ya fedha hizo , kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3 kimetengwa kwa ajili ya
matumizi ya kawaida,ikijumuisha shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya
watumishi wa serikali ,taasisi na wakala za serikali na shilingi bilioni 1,910.4 kwa ajili ya
mfuko mkuu wa serikali.Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo,ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,054.1 ni
fedha za nje.
94. Mheshimiwa Spika, kutokana na  maelezo ya mfumo wa bajeti yaliyotolewa hapo
juu ,sura ya bajeti kwa mwaka 2011/12 itakuwa kama ifuatayo:
MAPATO                                          Shilingi milioni
A:Mapato ya ndani                                     6,775,952
       (i)Mapato ya kodi (TRA)                      6,228,836
       (ii)Mapato yasiyo ya kodi                         547,116
B:Mapato ya halmashauri                                350,496       
C:Mikopo na misaada  ya nje                           3,923,551    
D:Mikopo ya ndani                                          1,2o4,262   
E:Mikopo  ya masharti ya kibiashara              1,271,634  
JUMLA YA MAPATO  YOTE                  13,525,895
F:Matumizi ya kawaida                                 8,600,287
        (ii)Mfuko mkuu wa Serikali                   1,910,376
        (ii)Mishahara                                           3,270,292
        (iii)Matumizi Mengineyo                        3,419,619
              Wizara                                                 2,727,472
              Mikoa                                                   49,981
             Halmashauri                                           642,166
G:Matumizi ya Maendeleo                                 4,924,608
     (i) Fedha za Ndani                                          1,871,471
     (ii) Fedha za Nje                                              3,054,137
JUMLA YA MATUMIZI YOTE                       13,525,895Hitimisho 
95. Mheshimiwa Spika,Bajeti ya mwaka 2011/12 ni mwendelezo wa juhudi za serikali
za kuwaletea maendeleo wananchi ,bajeti hii imezingatia:
(i) Dira ya taifa ya maendeleo 2025
 (ii) Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini awamu ya pili (MKUKUTA II)
(iii)Malengo ya Maendeleo ya millennia 2015
(iv)Ilani  ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2011/2015
(v)Mkakati wa pamoja wa misaada Tanzania  misaada Tanzania (MPAMITA)
(vi) Mkakati wa taifa wa madeni 
(vii) Sera za kijumla za Uchumi kwa mwaka 2011/12
96 Mheshimiwa Spika, Ili kufikia malengo hayo mapema zaidi ,kila mwananchi
anapaswa kujituma na kushiriki kikamilifu , kwa kutumia fursa zilizopo za kuzalisha mali
na kujiongezea kipato, ni matumaini yangu kuwa utekelezaji sahihi wa bajeti hii
utaiwezesha serikali kuwaletea wananchi  maendeleo tunayokusudia.
Bajeti ya mwaka 2011/12 imeandaliwa katika kipindi ambacho nchi yetu inakaliwa na
changamoto ya kiuchumi ikiwemo upungufu wa umeme na ongezeko la bei za mafuta
katika soko la dunia.
Hali hii imetishia ustawi wa uchumi na uwezo wa kukusanya mapato ya  ndani .serikali
imejipanga kukabiliana na changamoto hizi, ikiwa ni pamoja na kuharakisha miradi ya
uzalishaji umeme na uanzishwaji wa hifadhi kubwa ya mafuta yanayoagizwa ,wakati
serikali ikichukua hatua hizi ,wananchi wanaombwa kuanza kutumia kwa uangalifu
vyanzo vya nishati ,ili kupunguza gharama ,hivyo ni matumizi ya serikali kwamba bajeti
ya mwaka 2011/12 itatekelezwa kama ilivyopangwa
97 Mheshimiwa Spika Serikali ya awamu ya nne imedhamiria kwa kuendeleza misingi
imara ya kujenga uwezo katika kukusanya mapato ya ndani,hili litawezekana kwa
kuwekeza katika vichocheo vya ukuaji uchumi ili kuongeza wigo wa mapato ya ndani
kwa lengo la kutuongezea uwezo wa kujitegemea,kama nilivyoeleza hapo awali
,maeneo yafuatayo ya kimkakati yatazingatiwa katika mgao wa rasilimali katika muda
wa kati,nishati ya umeme,reli ,bandari,TEHAMA,Maji Kilimo na kulinda mafanikioa
yaliyopatikana katika sekta ya elimu na afya.Hivyo basi ,hatuna kila mmoja wetu kwa pamoja kuongeza ubunifu katika uzalishaji
wenye tija utakaoongeza pato la Taifa na hatimaye kuondokana na umaskini 
98 Mheshimiwa Spika ,Bajeti hii imezingatia ushauri wa waheshimiwa wabunge wa
kamati ya fedha na uchumi na makamti nyingine za kisekta.
Pia imezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbalimbali ,wakiwemo
wafanyabiashara,wenye viwanda,sekta ya kilimo,utalii na w engine wengi.Nawashukuru
wote hao kwa mawazo na ushauri wao
99 Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwashukuru wapiga kura wangu wote wa
jimbo la kilosa kwa kunichagua tena kuwa mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka
mitano.Napenda kuwaahidi kwamba tutashirikiana pamoja kuliletea maendeleo jimbo
letu la Kilosa.ninaamini kwamba sitawaangusha.mwisho nachukua pia nafasi hii
kumshukuru kipekee mke wangu mpendwa kwa kuwa msaada mkubwa kwangu.
100.Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza awali serikali inatambua makali ya maisha
yanayowakabili wananchi .kuna tatizo la upungufu wa umeme,kuongezeka kwa bei za
mafuta ya Petroli na gharama za usafiri,tatizo la ajira na haja ya kuboresha hifadhi yetu
ya chakula.Serikali sikivu ya chama cha mapinduzi imejipanga kikamilifu kukabiliana na
changamoto  hizo .Ni matumaini ya Serikali kwamba hatua za kukabiliana na
changamoto hizo nilizozieleza zitasaidia kuondoa kero hizo na hivyo kuboresha maisha
ya wananchi.
101. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja 

No comments: