ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 19, 2012

LINAH WAENDELEA NA KUJIFUA TAYARI KWA MAKAMUZI RENDEZVOUS



 Msaniii wa kizazi kipya Linah (kati) akiwa na madansa wake Helena Nyerere (kulia) na Julia Nyerere wakiwa kwenye mazoezi makali ya kujiweka sawa na show ya kukata na shoka itakayofanyikia Rendezvous, Rockville, MD wiki ya Pasaka April 7, 2012 show hii imeandaliwa na J&P wakishirikiana na DMK Global chini ya usaidizi wa Luke Music Factory na Itafunguliwa pazia na DirtyHerry akishirikiana na Cici akifuatiwa na AJ Ubao address ni 11910 Parklawn Dr, Rockville, MD
 Linah akiwa na madansa wake wakiendelea na amzoezi ya nguvu wakiandaa na show kabambe wiki ya Pasaka.
 Msanii Linah ujio wake upo chini ya Mhe. Letecia Nyerere Mbunge viti maalum (CHADEMA) ambae mbali ya Linah amesema anatarajia kuleta wasanii mbalimbali wa vizazi vipya katika kuutangaza muziki wao katika anga za kimataifa.
 Wakiwa kwenye mazoezi makali ya wimbo wa Bora Nikimbie ambao upo kwenye Album ya Atatamani ambayo iliyotoka 2011

Linah na madansa wake wameahidi show ya nguvu siku ya April 7, 2012 wamesema ukae mkao wa kula Pasaka kwa show na muziki ulioenda shule.

1 comment:

Anonymous said...

Let's go baibyyyy!!! do yo things.....