Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakimuogopi mwanachama wake yeyote kumdhibiti au kutomchukulia hatua za kinidhamu anapokwenda kinyume na sera au kukiuka taratibu husika.
Kauli hiyo itolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi, Issa Haji Usi Gavu, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana Kiswandui mjini hapa.
Alisema hoja ya kuwepo Muungano wa mkataba inakwenda kinyume na sera ya CCM na malengo ya Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Gavu alisema wanachama wote watakaokwenda kinyume na taratibu za kikatiba au kisera ana hakika wataadhibiwa kwa kufuata taratibu za kikatiba bila ya kukurupuka.
Alisema hakuna mwanachama yeyote ambaye ni maarufu kuliko CCM mbele ya katiba ya chama hicho na kuahidi kuwa vikao husika vitachukua maamuzi magumu wakati ukiwadia.
Aidha Gavu alisema sera ya CCM katika Muungano ni kuendelea na Serikali mbili na kwamba mwanachama anayetaka Muungano wa mkataba ana hiari ya kubaki au kujitoa.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya CCM uliotokana na mchakato wa utoaji wa maoni ya Katiba, Gavu alisema hakuna mgawanyiko wala mpasuko na kudai kuwa wanaosema hayo wamefilisika kisiasa.
Alisisitiza kuwa kama kuna wanachama ambao wamekwenda kinyume na mfumo wa kutii sera au katiba ya chama hicho ana hakika watahukumiwa kwa kufuata misingi ya maadili na kanuni za kinidhamu.
Kuhusu kuwepo kwa fununu za baadhi ya wanachama wa CUF na CCM wanaotaka Muungano wa mkataba kujiandaa kuanzisha chama kipya cha siasa alisema wako huru kufanya hivyo ili kutimiza kiu ya matakwa yao kidemokrasia.
"Si vizuri kupuuzia fufunu hizo, ikiwa wanaota ndoto ya kuanzisha chama cha siasa wana haki ya kufanya, wakijiona hawataki kukaa na majuha na kwamba wao ni werevu wajitoe ila CCM haitajuta," alisema Gavu.
Hata hivyo, katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema mgombea katika ngazi yoyote ya CCM na jumuiya zake atakaebainika kukiuka taratibu za uchaguzi ataadhibiwa kwa mujibu wa taraibu zilizowekwa.
Hivi karibuni kumeibuka baadhi ya viongozi wa CCM wakidai mfumo wa Muungano wa mkataba wakionekana kuungwa mkono na Jumuiya ya Uamsho na mihadhara (JUMIKI) ambayo inatetea Zanzibar kujitenga katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment